Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WILAYA ya Mpanda mkoani Katavi inakabiliwa na changamoto ya
wajawazito kufa kutokana na kutumia dawa za miti shamba kuongeza uchungu
wakati wa kujifungua.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mpanda , Dk Naibu Mkongwa alikiri
kuwa vifo vya wajawazito hospitalini hapo vinasababishwa na matumizi ya
dawa za kienyeji.
Alisema asilimia 90 ya wajawazito wanaokaribia kujifungua wanatumia
miti shamba kwa siri kujiongezea uchungu wa uzazi jambo linalohatarisha
maisha yao.
Alibainisha hayo hivi karibuni mbele ya wajumbe wa CCM wa Umoja wa
Jumuiya ya Wanawake (UWT) wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalumu wa mkoa
wa katavi , Anna Lupembe.
“Changamoto kubwa ni kuongezeka kwa idadi ya vifo vya wajawazito kila
mwezi kati ya vifo viwili hadi vinne lakini kwa wastani vitatu.
Nakumbuka mwaka 2012 kulikuwa na vifo 40 vya wajawazito. “Nisiwe mwongo
vifo hivyo vyote vingeweza kuzuilika, tatizo kubwa lililopo wananchi
wengi wanaamini dawa za kienyeji kuliko dawa zetu, asilimia 90 ya
wajawazito wanatumia dawa za miti shamba wanaposubiri kujifungua ili
wapate uchungu wa haraka,” alisema Dk Mkongwa.
Kuthibitisha hilo, alisema hivi karibuni walimkamata mhudumu wa afya
aliyekuwa akisubiri kujifungua hospitalini hapo akitumia dawa za miti
shamba za kuongeza uchungu wa uzazi.
Chanzo Gazeti la Habari leo

0 comments:
Post a Comment