Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
KATAVI YETU BLOG
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi limekamata silaha mbili za kivita aina ya SMG zikiwa na jumla ya risasi 62 na magazeni mbili pamoja na bunduki mbili aina ya gobore kabla ya kufanyika kwa tukio la ujambazikatika mnada wa mifugo ya ng-ombe katika Kata ya Simbesa Wilayani Mpanda .
Kaimu kamanda wa polisii wa Mkoa wa Katavi Rashid
Mohamed aliwaambia waandishi wa Habari hapo jana kuwa tukio hilo
lilitokea hapo jana majira ya saa tatu asubuhi huko katika kijiji cha Smbesa kata ya Simbesa.
Alisema watu wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na pikipiki moja aina ya Huonian rangi nyekundu yenye namba za usajiri T.948 BHU wakiwa wamebeba tenga la kubebea mizigo nyuma ya pikipiki walikutana na askari polisii wa doria.
Kaimu kamanda alieleza waliposimamishwa na porisi walikaidi agizo hilo na walianza kukimbia kwa kutumia pikipiki yao hiyo.
Askari baada ya kuona wamekaidi amri hiyo walianza kuwafukuza na walipokaribia kuwakamata walitelekeza pikipiki yao na kukimbia na kutokomea kusiko julikana kichakani .
Pikipiki hiyo baada ya kukaguliwa ilikutwa ikiwa na silaha mbili za kivita aina ya SMG huku zikiwa na risasi 62 na magazine zake zikiwa zimeviringishwa kwenye suruali ya jens na kufungwa kwenye tenga nyuma ya pikipiki.
Kaimu Kamanda Rashid Mohamed alisema watu hao walikuwa wamepanga kwenda kufanya ujambazi katika mnada wan g-ombe ambao ulikuwa ukifanyika katika kijiji cha Simbesa.
Katika tukio jingine lililitokea hapo juzi katika kijiji hicho cha Simbesa mtu mmoja alijulikana kwa jina la Ge4ofrey john 34 Mkazi wa Kijiji cha Nkungwi alikamatwa akiwa na silaha moja aina ya gobore huku akiwa nayo shambani kwake kwa lengo la kuwindia wanyama .
Pia polisi memkamata mtu mmoja alijulikana kwa jina la Donath Laulent 32 Mkazi wa Kijiji cha Simbesa akiwa na bunduki aina ya gobore akiwa ameificha kwa kuifadhi kwenye majani nje ya nyumba yake .
Kaimu kamanda Rashid Mohamed alisema jeshi
la polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta watuhumiwa waliotelekeza
pikipiki kwa kumtafuta mmiliki harali wa pikipiki hiyo ili kuweza
kuwabaini walikuwa na silaha hizo za kivita .
Ambapo watuhumiwa wawili walioatwa na gobole bado wanashikiliwa na polisi wanatarajiwa kufikishwa mahakamani ili wakajibu tuhuma zinazo wakabili .

0 comments:
Post a Comment