Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wa Mkoa wa Katavi Laulenti Mangeshi amenusurika kuvuliwa uongozi na kupewa onyo na na kikao cha mashauriano cha chama hicho cha Mkoa wa Katavi baada ya kubainika kuwa amekuwa amekuwa na makundi yanayosababisha mgawanyiko ndani ya chama na amekuwa akitowa lugha chafu kwa viongozi wenzake .
Mkutano ulioongozwa na Makamu Mwenyekiti Taifa upande wa Zanzibar Said Mohamed ulifanyika juzi katika ukumbi wa mikutano wa Inyonga Wilyani Mlele .
Mbali ya kikao hicho cha mashauriano cha Mkoa wa Katavi kumpa onyo Mwenyekiti huyo wa Mkoa pia
kiliwarudisha madarakani viongozi wa chama hicho wa Wilaya ya Mpanda
ambao walikuwa wamevuliwa uongozi na wanachama wa chama hicho kwa
kile walichodaiwa kukisaliti chama chao na kupelekea kupoteza jimbo la
Mpanda mjini lililokuwa likiongozwa na Said Arfi kwa vipindi viwili vilivyopita.
Viongozi waliorudishwa madarakani ni Mwenyekiti Mwenyekiti wa Chama hicho wa Wilaya ya Mpanda Abrahamu Mapunda ,Katibu wake Idd Faraji na viongozi wa chadema wa jimbo la Mpanda Mjini.
Wajumbe wa mkutano huo waliamua kuwarudisha madarakani baada ya kubainika kuwa utaratibu wa kuwaondoa viongozi hao haukufuata taratibu za chama hicho ingawa kulionekana kuwepo kwa mgogoro ndani ya chama hicho baina ya viongozi na wanachama.
Viongozi wa Wilaya ya Mpanda ya Mpanda na wa jimbo la Mpanda mjini walisimashwa uongozi na wanachama wao katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Katavi Resort mjini Mpanda hapo mwezi Novemba mwaka jana kikao ambacho kiliongozwa na viongozi wao wa kanda ya magharibi na kulikuwa na vurugu kubwa na ulinzi mkali wa askari polisi .
Kwa upande wa mwenyekiti wa Mkoa Laulent Mangweshi alikuwa
na wakati mgumu kutoka kwa wajumbe wa kikao hicho ambao wengi wao
walikuwa wakitaka avuliweuongozi kutokana na tuhuma zilizotolewa dhidi
yake .
Miomgoni mwa tuhuma hizo ni kuwa amekuwa akikigawa chama kwa kuwa na makundi na amekuwa akiwatolea lugha chafu viongozi wenzake na amekuwa akikiuka katiba ya chama hicho.
Kikao hicho kiliamua kumpa onyo na kumtaka asirudie tena makosa hayo na endapo atarudia tena atavuliwa uongozi bila kusubiri kikao chochote cha kumjadili.
Makamu mwenyeti wa Taifa upande wa Zanzibar Said Mohamed aliwataka wanachama na viongozi wa chama hicho kurudisha mshikamano ndani ya chama hicho .
Alisema miongoni mwa mikoa ambayo ilikuwa inafanya vizuri kwenye maswala ya uchaguzi Mkoa wa Katavi ulikuwa ni mkoa wa
juu lakini sasa hivi miongoni mwa mikoa ambayo imefanya vibaya kwenye
matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita mkoa huo ni mmoja wapo .
Mkoa wa Katavi unajumla ya majimbo ya uchaguzi matano na chama hicho hakikufanikiwa kupata mbunge hata mmoja na kina madiwani wane katika Mkoa mzima wa Katavi walipata katika majimbo yam panda vijijiji na Nsimbo.
0 comments:
Post a Comment