Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mtoto aliyejulikana kwa Jina la Nchimbi Tungu(11) Mkazi wa Kata ya Usevya Wilaya ya Mlele ameuwawa kikatili na Mama yake mzazi Sado Roketi (26) Mkazi wa Kata hiyo kwa kumpiga na fimbo katika sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha kumning’iza juu ya mti wa mwembe baada ya kumfunga kamba shingoni.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa
Habari kuwa tukio hilo na mama kuuwa mtoto wake wa kumzaa lilitokea
hapo juzi mida ya saa sita mchana kijijini hapo .
Siku hiyo ya tukio marehemu alipewa nguo na mama yake ili aweze kumfulia hata hivyo mtoto huyo hakuweza kufua nguo za mama yake kwa kile alichodai kuwa alikuwa amechoka .
Kamanda Kidavashari alisema ndipo mama wa marehemu alipokasirika na kuchukua fimbo na kuanza kumpiga kwa kushambulia sehemu mbalimbali za mwili wake huko mtoto huyo akiwa anapiga mayowe ya kuomba msaada na akimsihi mama yake amwachie.
Pamoja na marehemu kuomba msamaha kwa mama yake hakujari ombi la kuombwa msamaha na aliendelea kumpiga kwa kutumia fimbo licha ya marehemu kuendelea kulia.
Kamanda Kidavashari alieleza baada ya kugundua mtoto huyo amefariki Dunia kutokana na kichapo alichompa Sodo Roketi alimchukua mtoto marehemu huyo na kwenda nae kwenye mti wa mwembe na kisha alimfunga kamba na kumning’iza juu ya mti wa mwembe kwa lengo la kupoteza ushahidi.
Baada ya kuwa amemtundika juu ya mti aliendelea kufanya shughuli zake kama kawaida kwa ili watu wasimtilie shaka kuhusiana na mauwaji hayo .
Kidavashari alisema Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa Sado Roketi na anaendelea kuhojiwa na mara upelelezi utakapo kamilika anatarajiwa kufikishwa Mahakamani ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili
0 comments:
Post a Comment