Home » » MANISPAA YA MPANDA KUZINDUA MPANGO MKAKATI WA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

MANISPAA YA MPANDA KUZINDUA MPANGO MKAKATI WA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Manispaa ya Mpanda  Mkoani  Katavi   Desemba saba  inatarajia  kuzindua   mpango mkakati wa usafi na  utunzaji wa mazingira  na upandaji wa miti   
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda   Selemani  Lukanga  aliwaambia waandishi wa Habari juzi ofisini  kwake   kuwa  uzinduzi huo wa aina yake utafanyika katika  uwanja wa   Azimio   mjini  hapa  na  mgeni  Rasmi  atakuwa ni  Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr  Ibrahimu  Msengi
 Alisema  Manispaa hiyo  imeweka  mpango mkakati  wa utunzaji wa  mazingira na upandaji wa miti  katika  maeneo   yote ya Manispaa hiyo ya Mpanda
 Alifafanua  kuwa  Manispaa  inayo mikakati   ya  usafi wa mazingira  na wamekuwa  wakiitekeleza  na wamekuwa wakipata ushindi  wa  Kitaifa wa utunzaji wa mazingira  hivyo wanaenda  sambamba  na  gizo  la Rais  John Magufuli  alilo litowa hivi  karibuni la utunzaji wa mazingira
 Lukanga   alieleza  watatumia uzinduzi huo  kuweza kujipima  toka  Halmashauri hiyo ilianzishwa mwaka 2007 ikiwa Halmashauri ya Mji na  sasa Manispaa  wamefanikiwa kwa kiasi gani  katika usafi na utunzaji wa mazingira  na pia   wamepanga kujipanga kama Manispaa  kwani hapo  awali walikuwa ni Halmashauri ya Mji na sasa Nimaspaa kuanzia Julai  mwaka huu
 Alisema  lengo pia la uzinduzi huo  ni kuwafanya wadau mbalimbali  waweze kushiriki kwa vitendo  katika  shughuli za usafi na utunzaji wa mazingira na kuwafanya wananchi  wapende usafi
Lukanga  alieleza siku  hiyo  ya uzinduzi wananchi na Taasisi  mbalimbali  za  Manispa ya Mpandawatashiriki  kwenye zoezi    la  kufanya usafi  wakiwa  wameongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Dr Ibrahimu  Msengi
 Alisema  Mkuu wa Mkoa   kwenye uzinduzi huo  atakabidhi pikipiki  mbili kwa  Maafisa wa Afya wa Manispaa ya  Mpanda   zilizo  tolewa zawadi kwa Manispaa hiyo  baada ya kuwa  washindi wa utunzaji wa mazingira Kitaifa  na pia atakabidhi cheti cha ushindi kwa kijiji cha Kamakuka  kilichopo  katika Manispaa ya  Mpanda kwa kuwa washindi wa kwanza wa ujenzi wa vyoo vya kisasa hapa Nchini

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa