Home » » WALIOKUWA RAIA WA BURUNDI WAIOMBA KUBADILISHIWA HADHI YA MAKAZI

WALIOKUWA RAIA WA BURUNDI WAIOMBA KUBADILISHIWA HADHI YA MAKAZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter Muluchuma
Katavi
Waliokuwa  Raia wa Nchi ya Burundi  ambao hivi karibuni wamepewa uraia wa Tanzania
wanaoishi kwenye Makazi  ya Wakimbizi ya Mishamo Wilayani Mpanda  wameiomba Serikali   kuharakisha mchakato  wa  kubadili  hadhi ya Makazi hayo  kutoka makazi ya wakimbizi  kuwa  maeneo  maeneo yanayoendeshwa chini ya Serikali  za  Mitaa kama yalivyo maeneo mengine ya Tanzania
Ombi la  Raia wapya wa Tanzania  lilitolewa hapo  jana kwenye risala yao  iliyosomwa na  Agustino Thabiti  mbele ya Waziri  Mkuu Mizengo Pinda  wakati wa sherehe  zilizoandaliwa   na Raia hao wapya  waliokuwa wakiishukuru Serikali ya Tanzani kwa kuwapatia Urai  watu  Tanzania watu  wapatao 52,594 zilizofanyika katika uwanja wa Mishamo
 Walieleza lengo la kubadili makazi hayo   ni kurahisisha  upatikanaji  wa hudumu  za jamii  na utenganisho  wao  na jamii inao wazunguka
 Kufuatia  kutangazwa  kwa maeneo mapya  ya kiutawala  katika  ngazi ya  Tarafa ,Kata  na Vjiji mwezi june  2015 wanaishukuru Serikali  kwani kutokana na tangazo hilo  tayari wameshiriki kwa mara ya kwanza  kupiga kura ya kuwachagua Viongozi  katika uchaguzi  wa    Mkuu  wa oktoba 25 mwaka huu
 Na katika  uchaguzi huo  wamepata  Madiwani wanne  katika Kata nne zilizopo  kwenye Makazi hayo  ya Wakimbizi ya Mishamo yalionzishwa  mwaka 1978  hivyo wanaishukuru Serikali ya Tanzania  kwa kuendelea  kuongeza maeneo  mapya ya kiutawala
Pia waliiomba  Serikali kuona umuhimu  wa kuwasogezea   huduma  za Kibenki  kwani mahitaji  yao ni makubwa  kwa ajiri ya usalama wao na  fedha zao  hivyo wanalazimika kufuata huduma   za  kibenki  mjini Mpanda umbali wa kilometa  145  na   Mkoa wa jirani wa Kigoma
Kwa upande wake Waziri Mkuu Mizengo Pinda  alisema  Serikali ya Tanzania  namna  ya kuwafanya  watu hao walipewa vyeti vya uraia wa Tanzania  ili waweze kuishi  vizuri kama raia wengine
 Alisema  wapo  watu  3700 ambao ni Raia wa Nchi ya Burundi wanaoishi kwenye makazi hayo  waliomba kupatiwa uraia wa Tanzania   lakini wameshindwa  kupatiwa uraia kutokana na taratibu zao kutokamilika  hivyo ni vizuri  wakamilishe  taratibu  ili nao waweze kupatiwa uraia kama wenzao
 Alifafanua  wapo   watu 75 waliomba kurudi Nchini kwao Burundi  lakini  mpaka sasa watu hao bado wanaendeleea kuishi kwenye makazi hayo na baadhi yao wamegunduliwa kuwa sio Raia wa Burundi  mbali ni Raia wa Nchi ya Kongo hivyo kama wameamua  kuishi hapa nchini wafuate  taratibu  vinginevyo Serikali itawachukulia hatua

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa