Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Katavi
Msafara wa
mgombea wa Urais(CCM) Dk John
Magufuli ulilazimika kusimama
katika Vijiji vitatu
tofauti hapo jana wakati ukiwa unatokea Mjini Mpanda
kuelekea Mishamo wilayani
hapa baada ya wananchi wa vijiji
hivyo waliokuwa wamejipanga kwa wingi barabarani na kuuzuia msafara huu ili
waweze kumwona Dk Magufuli
Msafara huu wa mgombea Urais ulianza kusimamishwa
katika Kijiji cha Majalila
hali ambayo ililazimu msafara huu usimame na kumfanya Dk
Magufuli aamue kusimama
katika gari lake na kuwasalimia wananchi hao na kuwahaidi
endapo atachaguliwa atahakikisha
anamaliza kero za Wananchi hao kwani zinatambulika
Hali
kama hiyo ilitokea tena
kwenye vijiji vilivyokuwa mbele vya Nkondwe na
Luhafe ambako alikuta wananchi
wakiwa wamejipanga kwa wingi kando ya barabara huku wakiwa na shauku ya
kumwona hari ambayo ilipelekea msafara huu usimame na Dk
Magufuli kulazimika kusimama na kuwahutubia mamia ya wananchi hao
walikuwa wamesimama kando ya barabara
Mgombea huyo wa Urais(CCM) alipokuwa akiwahutubia
maelfu ya Wananchi waliokuwa Raia wa Nchi ya Burundi ambao wamepewa Urai
wa Tanzania katika Kijiji cha
Mishamo aliwahakikishia kuwa Serikali yake
ijayo ya awamu ya tano
itahakikisha inawaboreshea miundo mbinu mbalimbali
Alisema
Serikali yake itajenga barabara
kwa kiwango cha rami barabara yenye urefu wa kilometa 199
inayotoka Mpanda hadi uvinza Mkoani Kigoma
Pia itajenga zahanati kila kijiji na kila kata atahakikisha wanajenga kituo cha afya na kila
Wilaya Hospitali na kila Mkoa Hospitali ya Rufaa
Vilevile Serikali
yake itatowa elimu bure kuanzia shule ya
Msingi hadi sekondari na itaboresha makazi ya
nyumba za kuishi waalimu na itaboresha huduma ya maji na kufikisha nishati ya umeme kwa yale maeneo
ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo
0 comments:
Post a Comment