Home » » KATAVI: FUSO LA GONGANA NA BASI NA KUUWA MMOJA NA KUJERUHI SABA‏

KATAVI: FUSO LA GONGANA NA BASI NA KUUWA MMOJA NA KUJERUHI SABA‏

 Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Mtu mmoja amefariki dunia  hapo hapo Wilayani  Mlele   Mkoani  Katavi  baada ya  gari  Roli aina ya Fuso alilo kuwa  akisafiria   kugongana  na basi la Kampuni ya SBS  na watu wengine saba  kujeruhiwa
Kwa mujibu wa Kamanda wa jeshi la polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  ajali hiyo ilitokea hapo jana majira ya saa  moja na nusu  jioni  katika  eneo la  Kakuni  Kata ya Kibaoni  Wilaya ya  Mlele  Mkoani hapa
 Kidavashari  alimtaja  marehemu aliyefariki Dunia kwenye ajari hiyo kuwa ni   Gerald  Thadeo  (Kavunila)23 Mkazi wa Kijiji cha Kibaoni Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele
Alisema  hiyo  ilihusisha  magari yenye namba za  usajiri T .538 aina ya Fuso   mali  ya Jofrey  Pinda lililokuwa likiendeshwa na Braison Makangata (35) Mkazi wa Kijiji cha Kibaoni   na  Basi   lenye  namba za usajiri  T .223 ATW aina ya Scania mali ya kampuni ya SBS
Kidavashari alieleza  Roli hilo lilikuwa limewapakia wachezaji wa timu ya mpira  wa miguu  ya kibaoni   ambao walikuwa wametoka kucheza  mchezo wa mpira wa miguu wa kirafiki  katika kijiji cha jirani cha Usevya hivyo wakati walipokuwa wakirudi  ndipo walipofika kwenye Eneo la Kakuni  Roli hilo lilipogongana na  basi la Kampuni ya SBS ambalo lilikuwa likitokea Wilayani Mpanda  kuelekea majimoto  Tarafa ya Mamba na kusababisha kifo hicho  na majeruhi saba
Aliwaja  majeruhi hao kuwa ni Pinda  Offu(21) Alkizanda  Mapelani ,Ericki  Ulaya(20) Mashaka Mapelani (31)Furaha  Lusambo (20)   Michael  Kasanga (25) na Charles  zuya (23) wote wakazi wa Kijiji cha Kibaoni
Majeruhi  wote hao saba  walipatiwa  matibabu  katika   zahanati ya  Kibaoni  na kuruhusiwa  kwenda   nyumbani  kutokana  na  afya  zao  kuwa nzuri
 Alisema chanzo  cha ajari hiyo kilitokana na mwendo kasi wa  magari hayo yote mawili  na  ametowa wito kwa wamiliki  wa magari na madreva  wanaoendesha vyombo vya moto kufuata  sheria za usalama barabarani  ikiwa ni pamoja na kufanyia matengenezo   magari  yao  ili waweze kuepusha  na ajari


       
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa