Na Walter
Mguluchuma
Katavi Mtu mmoja amefariki dunia hapo hapo Wilayani Mlele Mkoani Katavi baada ya gari Roli aina ya Fuso alilo kuwa akisafiria kugongana na basi la Kampuni ya SBS na watu wengine saba kujeruhiwa
Kwa mujibu wa Kamanda wa jeshi la polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari ajali hiyo ilitokea hapo jana majira ya saa moja na nusu jioni katika eneo la Kakuni Kata ya Kibaoni Wilaya ya Mlele Mkoani hapa
Kidavashari alimtaja marehemu aliyefariki Dunia kwenye ajari hiyo kuwa ni Gerald Thadeo (Kavunila)23 Mkazi wa Kijiji cha Kibaoni Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele
Alisema hiyo ilihusisha magari yenye namba za usajiri T .538 aina ya Fuso mali ya Jofrey Pinda lililokuwa likiendeshwa na Braison Makangata (35) Mkazi wa Kijiji cha Kibaoni na Basi lenye namba za usajiri T .223 ATW aina ya Scania mali ya kampuni ya SBS
Kidavashari alieleza Roli hilo lilikuwa limewapakia wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya kibaoni ambao walikuwa wametoka kucheza mchezo wa mpira wa miguu wa kirafiki katika kijiji cha jirani cha Usevya hivyo wakati walipokuwa wakirudi ndipo walipofika kwenye Eneo la Kakuni Roli hilo lilipogongana na basi la Kampuni ya SBS ambalo lilikuwa likitokea Wilayani Mpanda kuelekea majimoto Tarafa ya Mamba na kusababisha kifo hicho na majeruhi saba
Aliwaja majeruhi hao kuwa ni Pinda Offu(21) Alkizanda Mapelani ,Ericki Ulaya(20) Mashaka Mapelani (31)Furaha Lusambo (20) Michael Kasanga (25) na Charles zuya (23) wote wakazi wa Kijiji cha Kibaoni
Majeruhi wote hao saba walipatiwa matibabu katika zahanati ya Kibaoni na kuruhusiwa kwenda nyumbani kutokana na afya zao kuwa nzuri
Alisema chanzo cha ajari hiyo kilitokana na mwendo kasi wa magari hayo yote mawili na ametowa wito kwa wamiliki wa magari na madreva wanaoendesha vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kufanyia matengenezo magari yao ili waweze kuepusha na ajari
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment