Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia mganga
mmoja wa Jadi kwa tuhuma za kumkamata
akiwa na ngozi mbili za chui na mkia wa
nyumbu akiwa amehifadhi ndani ya chumba chake cha kulala
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri alimtaja mtuhumiwa
huyo aliyekamatwa na nyara hizo
za Serikali kuwa ni Kabichi Nhulu
(39) Mkazi wa Kijiji cha Kakese Tarafa ya Misunkumilo Wilaya ya Mpanda Mkoani hapa
Alisema tukio la kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo
lilitokea hapo jana majira ya saa kumi na mbili jioni nyumbani kwa mthumiwa
katika Kijiji cha Kakese
Alifafanua kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa kufuatia taarifa za kilizotolewa kwa jeshi la polisi kutoka
kwa raia wema kuwa mtuhumiwa
huyo anamiliki nyara za
Serikali visivyo alali
Alieleza baada ya taarifa hizo kulifikia jeshi
la polisi lilifika kijijini hapo kwa
lengo la kufanya upekuzi kwenye nyumba
ambayo anaishi mtuhumiwa huyo
Kidavashari alisema baada ya polisi kufanya upekuzi ndani ya
nyumba ya mtuhumiwa Kabichi Nhulu
alikamatwa akiwa na ngozi mbili za chui na mkia wa nyumbu akiwa amehifadhi
ndani ya chumba chake cha kulala akiwa ameficha chini ya uvungu wa kitanda
Mtuhumiwa
anaendelea kushikiliwa na
jeshi la Polisi
kwa mahojiano zaidi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani
baada ya upelelezi
kukamilika ili aweze kujibu
tuhuma inayomkabili
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment