Home » » PINDA MSICHAGUE VIONGOZI WANAOTOWA RUSHWA

PINDA MSICHAGUE VIONGOZI WANAOTOWA RUSHWA


Na  Walter Mguluchuma
Katavi
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewataka  wananchi wa Tanzania kutowachagua  watu wanataka kugombea Urais  Ubunge na Udiwani  ambao  wanataka uongozi huo kwa  njia ya kutowa   pesa (RUSHWA) kwa wananchi  bali wawachague watu ambao wanaweza kuwaongoza
  Pinda alitowa kauli hiyo hapo jana wakati alipokuwa akiwahutubia  maelfu ya wananchi wa Tarafa  ya Inyonga Wilayani Mlele Mkoani Katavi  kwenye mkutano wa hadhara   uliofanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Inyonga
Alisema wako watu wanaotaka uongozi  kwa njia ya kuwapatia  wananchi pesa (RUSHWA) watu wananma  hiyo hawafai kuwa  wagombea wa Urais ,ubunge na udiwani  katika Nchi hii
Alieleza   hakikisheni nyinyi wananchi  mnachagua viongozi ambao  wanaweza kuwaogoza  kwenye  maeneo yenu na  sio vinginevyo achaneni na watu wanaowapa  pesa  
 Alisema hao watu wanaotaka uongozi kwa njia ya pesa  wakiwaletea hizo pesa   kuleni tuu lakini  hakikisheni  wakati wa  uchaguzi  msiwape  kura zenu  alisema  huku akishangiliwa na wananchi hao kwa kupigiwa  makofi na vigelegele
Alifafanua  ukitaka  kumchagua mtu mwenye sifa  anaefaa  kuwa Rais wa nchi hii  mchague mtu  ambae hatowi Rushwa  kwa wananchi 
 Alisema hata kwa watu ambao wanataka  ubunge na udiwani  hakikisheni hamuwachaguwi wale watu wanaotaka  uongozi kwa kuwapatia pesa ili  muwape kura  bali  chagueni viongozi watakao waongoza  vizuri  kwenye maeneo yenu
 Pinda   ambae pia ni Mbunge wa jimbo la Katavi  alitumia  nafasi hiyo kuwaambia  wananchi hao kuwa yeye  hata gombea ubunge   wa jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu baada ya kuliongoza   jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 15
Alieleza  wakati wa yeye kuendelea kuwa  mbunge wa jimbo hilo  umetoshs hivyo  sasa  anatafuta  kitu  kingine   sio ubunge  tena  alisema  waziri Mkuu Pinda
 Katika mkutano huo  wananchi walifika kwenye mkutano huo huku wakiwa na mabango  yalikuwa yameandikwa ujumbe   mbalimbali  baadhi ya mabango yalikuwa yameandikwa Pinda Kimya kimya hadi Ikulu mwaka 2015
Pinda pia alitowa wito kwa wananchi  wajitokeze kwa wingi  kwenye kujiandikisha  kwenye  daftari  la wapiga kura ambapo  zoezi hilo  linatarajia  kuanza hivi karibuni
 Alisema watu wote waliofikia umri wa miaka 18 wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari hilo la wapiga kura bila  kujali itikadi za vyama vya siasa
 Alifafanua  endapo mtu atashindwa kujiandikisha atakuwa amekosa haki yake ya msingi ya kuchagua viongozi wake watakao muongoza kwa kipindi cha miaka mitano
 Alisema   watu wasipo jiandikisha  kwenye daftari la wapiga kura  kunawafanya watu wachache  wawachague  viongozi  hata ambao hawafai  na kuwaogoza kwenye maeneo yao
 Pinda pia  alitaka viongozi wa Chama cha Mapinduzi  kuwateuwa watu  wanaofaa  kugombea uongozi kwenye nafasi mbalimbali  wale ambao wanakubalika na wananchi
 Alisema kumekuwepo na tabia ya  kuteuwa watu  ambao hawakubaliki  kwa wananchi  na matokeo yake  watu hao wamekuwa  wakishindwa kwenye uchaguzi  acheni chuki msiteuwe watu kugombea kwa ajiri ya kupewa pesa na urafiki
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa