Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Waziri Mkuu
Mizengo Pinda amewataka wakazi wa Mkoa wa Katavi kuhakikisha wanawafundisha uzalendo
wa Nchi yetu waliokuwa Raia wa
Burundi wanaoishi katika makazi ya wakimbizi ya Katumba na Mishamo yalioko
Mkoani Katavi ambao hivi karibuni wamepewa
uraia wa Tanzania na Serikali hivi karibuni
Pinda alitowa
wito huo hapo jana wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Tarafa ya
Nsimbo kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya
msingi Songambele
Alisema
Serikali imeanza kutoa urai kwa
wakimbizi wa kutoka nchi ya Burundi wanaoishi kwenye
makazi ya wakimbizi ya Katumba Wilayani
Mlele na Mishamo Wilayani Mpanda
Pinda alieleza makazi hayo ya wanayo ishi raia wa nchi ya Burundi wapatao zaidi ya laki mbili ambapo Makazi ya Katumba wapo Raia hao wa Burundi
84,000 na makazi ya Mishamo wako 200,000
Alieleza
idadi ya Raia hao wa Burundi wanaopewa uraia ni kubwa ukilinganisha na idadi ya wakazi wa
Mkoa wa Katavi kwa ujumla wake ambapo unawakazi laki tano
Alisema
ilikujiandaa na changamoto ya rai hao ni
vizuri wananchi wa Mkoa wa Katavi
wakajiandaa na changamoto hiyo hivyo
wanaowajibu wa kuwafundisha uzalendo wa Tanzania Raia hao wapya ili
waipende Nchi yetu
Aliwafafanulia kuwa endapo raia hao
hawatafundishwa uzalendo bado wataendelea
kuwa na fikira za kuwazia nchi yao ya Burundi badala ya kuiwazia nchi
yao mpya ya Tanzania
Pinda aliwataka rai hao wapya wa kutoka nchi ya
Burundi kuhakikisha wanaendeleza amani na utulivu wa Nchi yetu kwani Tanzania
ni nchi ya amani
Ogopeni sana watu ambao wanataka kuvunja amani
ya nchi yetu kwani mara nyingi vita inapo tokea wanaoathirika zaidi ni watoto
,wazee na walemavu na watanzania hata
vita ikitokea hata mahali kwa kukimbilia hawajuwi kwa kuwa hatuja zowea vita alisema
Pinda
Pia waziri
mkuu Pinda aliwataka wakulima wa Tumbaku wa Katavi kuakikisha wanatumia
vizuri fedha zao wanazozipata kutokana na mauzo yao ya tumbaku ili waweze
kubadilisha maisha yao
Aiisema Wilaya ya Mlele peke yake wakulima wa
tumbaku wamejipatia kiasi cha shilingi Bilioni 10 huku Halmashauri zake mbili
zikiwa zimepata ushuru wa shilingi bilioni mbili kutoka kwa makampuni mawili
yanayonunua tumbaku Mkoani Katavi
Alisema tumieni fedha hizo kwa ajiri ya
maendeleo yenu jengeni nyumba bora na somesheni watoto wenu na sio kutumia
fedha hizo mnazopata kwa ajiri ya kuongeza wake
aliwaambia Pinda
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment