Thursday, January 8, 2015

PINDA ATAKA RAIA WAPYA WA BURUNDI WAFUNDISHWE UZALENDO


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewataka wakazi wa Mkoa wa Katavi kuhakikisha wanawafundisha  uzalendo  wa Nchi yetu  waliokuwa Raia wa Burundi wanaoishi katika makazi ya wakimbizi ya Katumba na Mishamo yalioko Mkoani Katavi ambao hivi karibuni wamepewa  uraia wa Tanzania na Serikali hivi karibuni
Pinda alitowa wito huo hapo jana wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Tarafa ya Nsimbo  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye  uwanja wa shule ya msingi Songambele
 Alisema  Serikali imeanza kutoa urai kwa   wakimbizi  wa  kutoka nchi ya Burundi wanaoishi kwenye makazi ya wakimbizi ya Katumba  Wilayani Mlele na Mishamo  Wilayani  Mpanda
 Pinda alieleza makazi hayo ya wanayo ishi  raia wa nchi ya Burundi  wapatao zaidi ya laki mbili ambapo  Makazi ya Katumba wapo Raia hao wa Burundi 84,000 na makazi ya Mishamo wako 200,000
 Alieleza  idadi ya Raia hao wa Burundi wanaopewa uraia ni  kubwa ukilinganisha na idadi ya wakazi wa Mkoa wa Katavi kwa ujumla wake ambapo unawakazi laki tano
Alisema ilikujiandaa na changamoto ya rai hao  ni vizuri wananchi wa Mkoa wa Katavi  wakajiandaa na changamoto hiyo hivyo   wanaowajibu wa kuwafundisha uzalendo wa Tanzania Raia hao wapya ili waipende Nchi yetu
 Aliwafafanulia kuwa endapo raia hao hawatafundishwa uzalendo bado wataendelea  kuwa na fikira za kuwazia nchi yao ya Burundi badala ya kuiwazia nchi yao mpya ya Tanzania
Pinda  aliwataka rai hao wapya wa kutoka nchi ya Burundi kuhakikisha wanaendeleza amani na utulivu wa Nchi yetu kwani Tanzania ni nchi ya amani
 Ogopeni sana watu ambao wanataka kuvunja amani ya nchi yetu kwani mara nyingi vita inapo tokea wanaoathirika zaidi ni watoto ,wazee na walemavu na watanzania   hata vita ikitokea  hata  mahali kwa kukimbilia  hawajuwi kwa kuwa hatuja zowea vita alisema Pinda
 Pia waziri  mkuu Pinda aliwataka wakulima wa Tumbaku wa Katavi kuakikisha wanatumia vizuri fedha zao wanazozipata kutokana na mauzo yao ya tumbaku ili waweze kubadilisha maisha yao
 Aiisema Wilaya ya Mlele peke yake wakulima wa tumbaku wamejipatia kiasi cha shilingi Bilioni 10 huku Halmashauri zake mbili zikiwa zimepata ushuru wa shilingi bilioni mbili kutoka kwa makampuni mawili yanayonunua tumbaku Mkoani Katavi
 Alisema tumieni fedha hizo kwa ajiri ya maendeleo yenu jengeni nyumba bora na somesheni watoto wenu na sio kutumia fedha hizo mnazopata kwa ajiri ya kuongeza wake  aliwaambia Pinda
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

No comments:

Post a Comment