Na Walter Mguluchuma
Katavi
Waziri Mkuu
Mizengo Pinda amewataka wananchi wa
Tanzania kutowachagua watu wanataka
kugombea Urais Ubunge na Udiwani ambao
wanataka uongozi huo kwa njia ya
kutowa pesa (RUSHWA) kwa wananchi bali wawachague watu ambao wanaweza
kuwaongoza
Pinda alitowa kauli hiyo hapo jana wakati
alipokuwa akiwahutubia maelfu ya
wananchi wa Tarafa ya Inyonga Wilayani
Mlele Mkoani Katavi kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika katika uwanja wa
shule ya Msingi Inyonga
Alisema wako watu
wanaotaka uongozi kwa njia ya
kuwapatia wananchi pesa (RUSHWA) watu
wananma hiyo hawafai kuwa wagombea wa Urais ,ubunge na udiwani katika Nchi hii
Alieleza hakikisheni nyinyi wananchi mnachagua viongozi ambao wanaweza kuwaogoza kwenye
maeneo yenu na sio vinginevyo
achaneni na watu wanaowapa pesa
Alisema hao watu wanaotaka uongozi kwa njia ya
pesa wakiwaletea hizo pesa kuleni tuu lakini hakikisheni
wakati wa uchaguzi msiwape kura zenu
alisema huku akishangiliwa na
wananchi hao kwa kupigiwa makofi na
vigelegele
Alifafanua ukitaka
kumchagua mtu mwenye sifa anaefaa
kuwa Rais wa nchi hii mchague
mtu ambae hatowi Rushwa kwa wananchi
Alisema hata kwa watu ambao wanataka ubunge na udiwani hakikisheni hamuwachaguwi wale watu
wanaotaka uongozi kwa kuwapatia pesa
ili muwape kura bali
chagueni viongozi watakao waongoza
vizuri kwenye maeneo yenu
Pinda
ambae pia ni Mbunge wa jimbo la Katavi
alitumia nafasi hiyo kuwaambia wananchi hao kuwa yeye hata gombea ubunge wa jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka
huu baada ya kuliongoza jimbo hilo kwa
kipindi cha miaka 15
Alieleza wakati wa yeye kuendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo umetoshs hivyo sasa
anatafuta kitu kingine
sio ubunge tena alisema
waziri Mkuu Pinda
Katika mkutano huo wananchi walifika kwenye mkutano huo huku
wakiwa na mabango yalikuwa yameandikwa
ujumbe mbalimbali baadhi ya mabango yalikuwa yameandikwa Pinda
Kimya kimya hadi Ikulu mwaka 2015
Pinda pia alitowa
wito kwa wananchi wajitokeze kwa
wingi kwenye kujiandikisha kwenye
daftari la wapiga kura
ambapo zoezi hilo linatarajia
kuanza hivi karibuni
Alisema watu wote waliofikia umri wa miaka 18
wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari hilo la wapiga kura bila kujali itikadi za vyama vya siasa
Alifafanua endapo mtu atashindwa kujiandikisha atakuwa
amekosa haki yake ya msingi ya kuchagua viongozi wake watakao muongoza kwa
kipindi cha miaka mitano
Alisema
watu wasipo jiandikisha kwenye
daftari la wapiga kura kunawafanya watu
wachache wawachague viongozi
hata ambao hawafai na kuwaogoza
kwenye maeneo yao
Pinda pia
alitaka viongozi wa Chama cha Mapinduzi
kuwateuwa watu wanaofaa kugombea uongozi kwenye nafasi mbalimbali wale ambao wanakubalika na wananchi
Alisema kumekuwepo na tabia ya kuteuwa watu
ambao hawakubaliki kwa wananchi na matokeo yake watu hao wamekuwa wakishindwa kwenye uchaguzi acheni chuki msiteuwe watu kugombea kwa ajiri
ya kupewa pesa na urafiki
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment