Na Walter Mguluchuma
Katavi
Waziri Mkuu
Mizengo Pinda ameziagiza Halmashauri
kuhakikisha zinapima viwanja kwa
ajiri ya ujenzi na kuvitenga kwa ajiri
ya watu wenye mahitaja maalumu kama vile wawekezaji na taasisi mbalimbali
Pinda alitowa
agizo hilo wakati wa sherehe za mkesha wa kuuwaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015 alikuwa
akiwahutubia wakazi wa Mkoa wa Katavi katika hotel ya Lyambalyamfipa mjini Mpanda
Alisema kuanzia
sasa Halmashuri zote hapa nchini ziwe na utaratibu wa kupima viwanja na
kuvitenga kwa ajiri ya makazi ya watu na kwa ajiri ya watu
wanaotaka kuweza kwa ajiri ya
ujenzi wa viwanda shule na Hospitali na majengo ya taasisi mbalimbali
Pinda alisema
imekuwa ni mazoea ya Halmashauri kutopima viwanja vya kutosha kwenye Halmashauri zao na matokeo yake imekuwa ikiwacheleweshea watu kuchelewa kupata viwanja wakati wanapokuwa
wanahitaji
Hivyo aliziagiza
Halmashauri kupima viwanja vya kutosha
ili watu wanapo vihitaji viwanja viwe
vinakuwa viko tayari
Alisema watu
wengi wamekuwa wakihitaji viwanja kwa ajiri ya ujenzi lakini wamekuwa wakijibiwa kwenye Halmashauri kuwa viwanja havija pimwa kwanini msipime viwanja vya kutosha ili wananchi
wanapo kuwa wanahitaji viwe vipo tayari kuliko kuwaambia wasubilie mpaka
vitakapo pimwa alisema Pinda
Alifafanua kuwa
kwa Halmashauri ambayo itakuwa iko tayari
kuomba mkopo wa fedha kwenye taasisi za kibenki kwa ajiri ya kupima viwanja ofisi yake iko tayari kutoa kibali cha kuombea mkopo huo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment