Saturday, January 3, 2015

PINDA SIJAWAHI WAHI KUPOKEA RUSHWA WALA KUTOA RUSHWA

Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Waziri Mkuu Mizengo  Pinda  amesema kuwa  yeye ni mtu mwadilifu  wala hajawahi kopokea rushwa  wala  kutowa rushwa kwa mtu yoyote yule katika maisha yake yote  na anahakika hata siku moja haita  tokea akakamatwa kwa kosa la rushwa  isipo kuwa kuna watu wanataka kumchafua  kwenye swala la IPTL kwa ajiri  ya kugombea Urais
Kauli hiyo   Pinda aliitowa  hapo jana wakati alipokuwa akiwahutubia  wananchi wa Mkoa wa Katavi wakati  wa sherehe  za kuuwaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015 zilizofanyika kwenye   Hotel  ya Lyambalyamfipa  Mjini  hapa
 Alisema  wako  baadhi ya watu  walikuwa wamepanga kumchafua kwa  kutaka  kumsingizia    kwenye kikao cha Bunge kilichomalizika hivi karibuni  mwezi wa  Novemba  kuwa  anahusika  na kashfa  ya uchotwaji wa  sh  bilioni  200 kwenye  Akaunt ya Tegeta Escrow
  Pinda  alisema  anawashanga sana watu ambao wanataka kumchafua kwa  kumsingizia  kuwa  yeye anahusika  katika  tuhuma za  pesa  tsh bilioni 200 kwenye  Akaunt ya  Tegeta  Ecsrow
 Alisema  yeye hausiki na wala hata husika  hata siku moja  kujihusisha  kwa kupokea Rushwa wala  kupokea  Rushwa kutoka sehemu yoyote   ile iwe ndani ya nchi au nje ya Nchi
 Swala hilo la yeye kutaka kuingizwa kwenye  tuhuma  za  IPTL  zilitokana na  mbio za kugombea Urais mwaka huu ndio watu wasio mtakia mema walipotaka kumchafua  kwa masilahi yao binafsi  na wahakikishia Tanzania wote  mimi ni mtu safi na mwandilifu  kwa serikali na kwa wanchi alisema Pinda
 Alisema   anashangazwa na kuhusishwa na kashfa  ya  IPTL  wakati hata   mmiliki wa kampuni ya  Harbinder Sing Seith hamfahamu wala hajawahi kumwona  katika maisha yake yote  kwa ujumla hamjui wala  hajawahi kuwa na mahusiano  yoyote yale nae wala kampuni yake
Pinda alieleza kuwa ataendelea kuwa mtii na mwaminifu kwa Riis  na na atajitahidi  kumsaidia  Rais  kufanya kazi  na ataendelea  kuwa mwadilifu  kwa Serikak na kwa wananchi wa Tanzania
 Alisema  anawashukuru sana  watu mbalimbali  waliompa pole kwa yale yaliotokea  wakati kikao cha Bunge  kilichomalizika Dodoma   mwezi  Novemba mwaka jana
 Alieleza mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho cha Bunge makundi mbalimbali   ya watu wa  ndani ya nchi na nje ya  yamekuwa yakimpa pore kwa  yale yaliotokea na wamemfanya  azidi kuwa na moyo wa kulitumika Taifa  kutokana na wanachi hao kuonyesha kuwa na imani nae
 Pinda alisema hata alipofika  Kijijini kwake  Kibaoni kwa ajiri ya mapumziko ya Krisimasi na mwaka mpya amekuwa akipokea watu mbalimbali kutoka Mkoa wa Katavi na Rukwa  walifika  nyumbani kwake kumpa pole
 Alisema hata juzi viongozi wa madhehebu yote ya dini yalioko katika Mkoa wa Katavi wamefika Kibaoni  kumpa pole  jambo ambalo amefarajika mmno  kuona viongozi wa dini walivyoguswa na swala hilo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

No comments:

Post a Comment