Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Waziri Mkuu
Mizengo Pinda amesema kuwa
yeye ni mtu mwadilifu wala
hajawahi kopokea rushwa wala kutowa rushwa kwa mtu yoyote yule katika
maisha yake yote na anahakika hata siku
moja haita tokea akakamatwa kwa kosa la
rushwa isipo kuwa kuna watu wanataka
kumchafua kwenye swala la IPTL kwa
ajiri ya kugombea Urais
Kauli hiyo Pinda aliitowa hapo jana wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Katavi wakati wa sherehe
za kuuwaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015 zilizofanyika
kwenye Hotel ya Lyambalyamfipa Mjini
hapa
Alisema
wako baadhi ya watu walikuwa wamepanga kumchafua kwa kutaka
kumsingizia kwenye kikao cha
Bunge kilichomalizika hivi karibuni
mwezi wa Novemba kuwa
anahusika na kashfa ya uchotwaji wa sh
bilioni 200 kwenye Akaunt ya Tegeta Escrow
Pinda
alisema anawashanga sana watu
ambao wanataka kumchafua kwa
kumsingizia kuwa yeye anahusika katika
tuhuma za pesa tsh bilioni 200 kwenye Akaunt ya
Tegeta Ecsrow
Alisema
yeye hausiki na wala hata husika
hata siku moja kujihusisha kwa kupokea Rushwa wala kupokea
Rushwa kutoka sehemu yoyote ile
iwe ndani ya nchi au nje ya Nchi
Swala hilo la yeye kutaka kuingizwa
kwenye tuhuma za
IPTL zilitokana na mbio za kugombea Urais mwaka huu ndio watu
wasio mtakia mema walipotaka kumchafua kwa masilahi yao binafsi na wahakikishia Tanzania wote mimi ni mtu safi na mwandilifu kwa serikali na kwa wanchi alisema Pinda
Alisema anashangazwa na kuhusishwa na kashfa ya
IPTL wakati hata mmiliki wa kampuni ya Harbinder Sing Seith hamfahamu wala hajawahi
kumwona katika maisha yake yote kwa ujumla hamjui wala hajawahi kuwa na mahusiano yoyote yale nae wala kampuni yake
Pinda alieleza
kuwa ataendelea kuwa mtii na mwaminifu kwa Riis
na na atajitahidi kumsaidia Rais kufanya kazi
na ataendelea kuwa mwadilifu kwa Serikak na kwa wananchi wa Tanzania
Alisema
anawashukuru sana watu
mbalimbali waliompa pole kwa yale
yaliotokea wakati kikao cha Bunge kilichomalizika Dodoma mwezi
Novemba mwaka jana
Alieleza mara baada ya kumalizika kwa kikao
hicho cha Bunge makundi mbalimbali ya
watu wa ndani ya nchi na nje ya yamekuwa yakimpa pore kwa yale yaliotokea na wamemfanya azidi kuwa na moyo wa kulitumika Taifa kutokana na wanachi hao kuonyesha kuwa na
imani nae
Pinda alisema hata alipofika Kijijini kwake Kibaoni kwa ajiri ya mapumziko ya Krisimasi
na mwaka mpya amekuwa akipokea watu mbalimbali kutoka Mkoa wa Katavi na
Rukwa walifika nyumbani kwake kumpa pole
Alisema hata juzi viongozi wa madhehebu yote
ya dini yalioko katika Mkoa wa Katavi wamefika Kibaoni kumpa pole
jambo ambalo amefarajika mmno
kuona viongozi wa dini walivyoguswa na swala hilo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment