Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Diwani wa Kata ya
Makanyagio (CHADEMA) katika Halmashauri
ya Mji wa Mpanda Idd Nzguye amemwahidi
Waziri Mkuu Mizengo kuwa atamlipia pesa za gharama za kuchukulia fomu za kugombea Urais
Nzguye alitowa ahadi hiyo hapo jana mbele ya
Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa sherehe za kuuwaga mwaka 2014 na
kuukaribisha mwaka 2015 zilizofanyika katika Hotel ya Lyambalyamfipa mjini
hapa
Alisema kuwa
ameridhishwa na utendaji wake wa kazi
hivyo utakapo fikia kipindi cha kuchukua fomu za kugombea Urais gharama ya fomu za kugombea Urais atalipa
yeye Diwani Nzguye
Alieleza
mbele ya umati wa watu
waliohudhuria sherehe hizo kuwa Mizigo
Pinda anaishi kwenye Kata yake ya Makanyagio hivyo
yeye kama Diwani wa Kata hiyo
ameamua kutoa ahadi ya kulimpia
gharama za pesa za kuchukilia fomu za kugombea Urais
Alisema ni
jambo la kujivunia kwake kuona
mgombea Urais anatoka kwenye kata yake
anayoiongoza hivyo ni wajibu wake
kumsaidia wananchi wake huyo ambae ni Pinda
Alisema sababu nyingine iliyomvutia mpaka
afikie uamuzi huo wa kumwahidi kulipia
fomu ya kugombea Urais ni jinsi ambavyo
Pinda hakuusika kabisa na tuhuma za kuchota fedha za IPTL
Nzguye alisema
haoni sababu yoyote ya kutomlipia fomu za kugombea Urais kutokana
na jitihada zinazofanywa na Pinda za
kusimamia shughuli za Serikali
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment