Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewataka wanawake
wote hapa Nchini waonapokuwa na dalili za kuwa na ungonjwa wa
tezi ya shingo ya uzazi salatani na
festula wawahi mapema hospitali ili
kuepukana na vifo vinavyotokana na
magonjwa hapo
Pinda alitowa
wito huo hapo juzi wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mji wa Mpanda
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Kashaulili
Mjini hapa
Alisema wanawake
wengi wamepoteza maisha kutokana
na chulewa kufika
hospitali kutibiwa ugonjwa wa
tezi ya shingo na festula na salatani wakati wangewahi kwenda hospitali magonjwa hayo yanatibika
Alifafanua
baadhi ya wanawake wamekuwa
wakiona aibu kwenda hospitali na kumwona Daktari
na kumweleza anaumwa nini ili aweze
kupatiwa msaada wa matibabu
Wapo wengine wanaogopa na kuona aibu kushikwa
matiti na Daktari wakati wanapimwa kansa
ya ziwa ugonjwa huo huwa
haugunduluki bila daktari kugusa chuchu za maziwa alisema Pinda
Alisema
yeye mwenyewe amekuwa
akiwapeleka akina mama wengi
ambao wamekuwa na matatizo hayo
lakini kila anapowafikisha
hospitali wamekuwa wakiambiwa kuwa
wamechelewa kufika hospitali na kupelekea kukatwa ziwa wakati wangewahi
wangeweza kupona
Pinda alisema
umefika wakati sasa wa akinamama
kubadilika na kuhakikisha
kila waonapo dalili za kuwa na
magonjwa hayo kuwahi mapema pindi
waonapokuwa na dalili za ugonjwa
Pia aliwataka
madaktari wote hapa nchini
kuwaelimisha wananchi na mapema madhara ya magonjwa hayo kwani wapo baadhi ya akina mama hawajuwi athari zake
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment