Na Walter Mguluchuma
Katavi yetu blog
Mwanamke mmoja alifahamika kwa jina la Minza Mwanalushinge (26) Mkazi wa Kata ya Kibaoni Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi ameuwawa kikatili kwa kukatwa katwa na mapanga viungo vyake na na kisha mwili wake kufukiwa chini ya ardhi shambani kwake
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina msaidizi mwandamizi Dhahiri Kidavashari mauwaji hayo ya kikatili yalitokea hapo juzi majira ya saa moja asubuhi huko katika kijiji cha Manga Kata ya Kibaoni
Siku hiyo ya tukio marehemu aliondoka nyumbani kwake majira ya saa kamili asubuhi kwenda kuchota maji kisimani umbali wa kilometa moja kutoka nyumbani kwake alikokuwa akiishi na mumewe aitwaye Kimbulu Joseph
Kamanda kidavashari alisema wakati marehemu akiwa anarudi nyumbani huku akiwa amebeba ndoo yake ya maji ndipo alikutana na watu wasio fahamika ambao walimshambulia kwa mapanga katika sehemu mbalimbali za mwili wake
Alieleza baada ya kuwa wamemshambulia marehemu hadi kufa wauwaji hao walianza kukatakata viungo vya mwili wa marehemu kwa kukata miguu yake na mikono kwa kuitenganisha na mwili wa marehemu
Kidavashari alisema kisha wauwaji hao waliuburuza mwili wa marehemu kutoka kwenye eneo hilo walilofanyia mauwaji hadi shambani kwa marehemu
Alieleza kisha wauwaji hao baada ya kuwa wameufikisha mwili huo wa marehemu kwenye shamba lake huku wakiwa wamekata viungo vya mwili wake walichimba shimo na kisha walimfukia marehemu ardhini pamoja na viungo vya mwili walivyokuwa wamevikata na kisha kutokomea kusiko julikana
Kamanda Kidashari alisema watu waliopita kwenye eneo la karibu na tukio walishitushwa kuona ndoo ya maji ikiwa imetupwa kichakani huku kukiwa hakuna mtu aliyeonekana kwenye eneo hilo zaidi ya damu zilizokuwa zimetapakaa hari ambayo iliwafanya waende kutoa taarifa kwa viongozi wa serikali wa kijiji hicho ambao nao walitowa taarifa kwenye kituo cha polisi cha Kibaoni
Polisi wa kituo cha Kibaoni walifika kwenye eneo hilo na ndipo walipokuta kuna mbuluzo ambao walilazimika kuufuata hadi uliko ichia kwenye shamba la marehemu na ndipo walipoweza kuona kuna kitu kinaonekana kufukiwa ardhini na walipofukua eneo hilo waliweza kuukuta mwili wa marehemu ukiwa umefukiwa ardhini huku ukiwa umekatwa miguu na mikono yake ambavyo vyote vilikuwa vimefukiwa kwenye shimo hilo pamoja na mwili wake
Kidavshari ameeleza kuwa jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi mpaka sasa ilina washikilia watu wawili kwa tuhuma za kuusika na mauwaji hayo ambao ni Kimbulu Joseph(52) ambae ni mume wa marehemu na Joseph Abel (35) mkazi wa Kitongoji cha Vilolo Kata ya Kibaoni Wilaya ya Mele
Watuhumiwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya uchunguzi utakapo kuwa umekamilika ili waweze kujibu tuhuma zinazowakabili
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment