Na Walter
Mguluchuma
Katavi yetu Blog
Jeshi la Polisi
Mkoa wa Katavi linamshikilia mtu mmoja
aitwaye Kanedeku Giti (26) Mkazi
wa Kijiji cha Minyoso
kata ya Kibaoni Wilaya ya Mlele
Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za
kumuuwa baba yake mzazi aitwaye Giti
Mawiti (53) kwa kumpiga na kitu kizito kichwani kutokana
imani za kishirikina akimtuhumu marehemu kumuuwa mtoto wake kwa ushirikina
Kamanda wa Jeshi
la polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri
Kidavashari alisema mbele ya
waandishi wa habari ofisini kwake kuwa
tukio hilo lilitokea hapo jana majira ya
saa tatu na robo usiku nyumbani kwa
marehemu
Alisema kabla ya tukio hilo marehemu alikuwa
nyumbani kwake huku akiwa anasumbuliwa
na ugonjwa wa kuumwa tumbo lake ambapo
baada ya kuona maumivu yanazidi kuwa
makali alilazimika kuwaamsha watoto wake watatu ambao alikuwa
akiishi nao ambao ni Kadeku Giti (26) Tupindo
Giti (21)na Nyanzobe Giti (16)
ili wamchemshie maji ya kunywea dawa
Alieleza
baada ya kuwa amewaamsha watoto
wake na kuwaagiza wamchemshie maji ya kunywea
dawa Marehemu aliamua k utoka chumbani kwake na kulala sebuleni wakati
akiwa anaendelea kusubilia maji ya
kunywea dawa ya kienyeji yachemke
Kamanda Kidavashari alisema ghafla alitokea
mtu mmoja huku akiwa amewasha
toshi yenye mwanga mkali ambayo iliwamulika machoni na kuwafanya watoto wa marehemu wa kimbie mbio kwenda kujificha kichakani huku wakiwa wamemuacha baba yao
akiwa amelala sebuleni
Wakati watoto wa marehemu wakiwa mafichoni
baada ya muda mfupi walisikia baba yao akipiga mayowe ya kuomba msaada kwa watoto
wake lakini kutokana na hofu waliokuwa
nayo walishindwa kurudi kutoa msaada kwa baba yao
Kamanda
Kidavashari alisema baada ya kuona hari
imekuwa kimya watoto wa marehemu
waliamua kurudi nyumbani na walimkuta
baba yao akiwa anagalagala chini
huku akiwa amepigwa na kitu kizito kichwani akiwa
anakoroma
Ndipo mtoto wake Kadeku Geti alipomuinua na kumbeba na kumpeleka
chumba kwake na kumlaza kitandani hata
hivyo baada ya muda si mrefu akwa amefariki Dunia
Alifafanua uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa kulikuwa chanzo cha
mauji hayo ni kutokana na ugomvi wa mara kwa mara baina ya marehemu na
mwanae Kanedeku Giti ambae alikuwa akimtuhumu baba yake kuwa alimuuwa mtoto wake kwa
imani za kishirikina
Alisema Polisi wanaendelea kumshikilia
mtuhumiwa Kanedeku Giti na upelelezi bado unaendelea na mara utakapo kamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati
wowote
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment