Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mkazi wa Kijiji
cha Masigo Kata ya Ilele Tarafa ya
Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa
Katavi Peter Kanyika (74) amefariki Dunia
baada ya kupata mshituko
alipopatataarifa ya kifo cha mke wa mtoto wake aliyefariki Dunia ghafla kwa
kupigwa na radi wakati akiwa shabani kwake
Kwa mijibu wa
mtoto wa marehemu Jackson
Shula ambae ni mtendaji wa Kijiji
hicho cha Masigo alisema tukio hilo la
kusikitisha la kifo cha baba yake na kifo cha mke wake
mdogo vilitokea wiki
iliyopita kwa nyakati tofauti
Alisema
baba yake mzazi huyo alifariki dunia
hapo Nonemba 28 katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda baada ya
kupata mshituko wa kifo cha mkwe wake
Siku hiyo ya tukio
ya tarehe 25 Novemba
majira ya saa nane na nusu mchana
huko katika kijiji cha Masigo mkwe wake
aitwaye Vaileti Mgude (25) ambae ni mke mdogo wa mtoto wake
Jackson Shula alikuwa shambani kwake akilima na kupanda mahindi
Wakati Vaileti
akiwa anaendelea na shughuli za
shamba akiwa na familia yakeghafla mvua ilianza
kunyesha hari ambayo iliwalazimu waache shughuli za shamba na kwenda
kukaa chini ya mti kwa ajiri ya
kujikinga na mvua
Alisema wakati wakiwa wamekaa chini ya mti Vaileti
akiwa na Wifi yake
Eni Bodoi huku akiwa amemlea mtoto wake mdogo aitwaye Pascal Mgude ndipo radi ilipo Mpiga Vaileti
kwenye sehemu zake za siri
kiunoni na shingoni na kumfanya
afariki Dunia hapo hapo na pia ilimrusha mtoto huyo ambae alikuwa amemlea na
kumjeruhi
Alisema baada ya radi hiyo kupiga majirani
walifika kwenye eneo hilo na kukuta
Vaileti akiwa amefariki Dunia huku mtoto wake
Pascal Mgude na Wifi yake na
marehemu Vaileti wakiwa wamejeruhiwa katika sehemu mbalimbali za mwili yao
Majirani
walilazimika kuwakimbiza majeruhi
hao na kuwapeleka katika kituo cha afya
cha Inyonga ambapo walilazwa na bado
wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye
kituo hicho hadi sasa
Jackson
alieleza ndipo Peter Kanyika
alipopata taarifa za kifo cha mke wa mtoto wake kilichotokana na kupigwa
na radi wakati akiwa shambani kwake
Taarifa hiyo ya ghafla ilimfanya Kanyika apate
mshituko na kisha alifunga kauli hari ambayo
iliwalazimu majirani na ndugu wa marehemu kumpeleka katika kituo cha
afya cha
Inyonga kwa ajiri ya
matibabu h
Alisema hari
ya Kanyika iliendelea kuwa mbaya na
alihamishiwa kwenye osipitali ya Wilaya ya Mpanda kwa ajiri ya matibabu zaidi hadi hapo
Novemba 28 alifariki Dunia wakati
akiwa anaendelea kupatiwa matibabu na
mazishi ya marehemu Kanyuka
yamlifanyika juzi katika makaburi ya
Inyonga Wilayani Mlele
Jeshi la Polisi
Mkoani Katavi limethibitisha kutokea kwa kifo cha mtu huyo aliyepigwa na radi katika Kijiji hicho
cha Masigo Wilayani Mlele
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment