Home » » WAKULIMA WA TUMBAKU KATAVI WAUZA TUMBAKU YENYE THAMANI YA ZAIDI YA DORA ZA KIMAREKANI MILIONI 28.7

WAKULIMA WA TUMBAKU KATAVI WAUZA TUMBAKU YENYE THAMANI YA ZAIDI YA DORA ZA KIMAREKANI MILIONI 28.7


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
 Wakulima wa Tumbaku wa Mkoa wa Katavi wameuza  zaidi ya kilo milioni  12.5  za  Tumbaku  zenye  thamani ya Dola  za Kimarekani  milioni  28,748,210 katika  msimu wa kilimi wa mwaka 2013 na 2014
Haya yalielezwa  katika  Risara ya wakulima wa Tumbaku  iliyosomwa na meneja  Mkuu wa  wa  chama kikuu cha   ushirika cha  wakulima wa Tumbaku cha Mkoa wa Katavi LATCU  Pius Kilo  wakati  wa  maadhimisho ya sherehe ya  kutimiza miaka 20 ya chama kikuu hicho yaliyofanyika kwenye viwanja vya Idara ya  Mjini Mpanda
Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho hayo alikuwa ni Waziri wa  kilimo na ushirika   mwandisi  Cristopher Chiza  ambae  aliwakilishwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi Paza Mwamlima
  Kilo  alisema  msimu wa kilimo wa   mwaka 2013 na 2014 wakulima wa Tumbaku  wa Mkoa wa Katavi wameweza   kuuza   kilo   12,577,306 za Tumbaku  zenye  thamani  ya Dola  za kimarekani  milioni  28,748,,210  ambapo   mkopo  wa pembejeo   ulikuwa  wa  thamani ya Dola  11,485,068 hivyo baada ya kulipa deni wakulima  walipata kiasi cha  dola  17, 263, 148  kwa hela za kitanzania ni sawa na shilingi Bilioni   27,621,028, 600 wastani kilo moja ilinunuliwa kwa bei ya tsh 1,600
Kwa  msimu wa kilimo wa mwaka 2014 na 2015 wakulima wanatarajia  kulima hekta 14,006 ambazo zinatarajia kuzalisha kilo  15,343,420 za Tumbaku  ambazo kwa wastani  wa msimu huu wa dola  mbili  kwa kilo  zinatarajiwa zitapatikana  dola  za Kimarekani  30,686,840 sawa  na  Tsh  shilingi Bilioni 49,098,944,000
 Alisema uzalishaji wa Tumbaku kwa msimu huu unatarajiwa kuongezeka  kutokana na  wingi wa wakulima  ubora wa zao hilo  na bei  kuwa  nzuri  ndio inafanya  kuwepo  na ongezeko  la uzalishaji  wa Tumbaku  katika Mkoa wa Katavi
Alitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili wakulima wa Tumbaku kuwa ni  uchache wa makampuni yanayo nunua Tumbaku  kuwa ni yaleyale  ya miaka yote wakati uzalishaji wa Tumbaku  imeongezeka  na wakati huo  makampuni yanayo nunua  Tumbaku yameanza  kupunguza  kasi  ya kununua Tumbaku
Changamoto nyingine  ni  sheria ya kusajiri  wa kulima wa kujitegemea  na kuanzishwa  kwa Association katika maeneo yenye vyama  vya ushirika  hari ambayo  inasafanya   kuwepo  kwa ulanguzi  na utoroshwaji wa Tumbaku   hivyo  husababisha vyama kushindwa  kulipa madeni kwenye taasisi  za kifedha  zilizowakopesha kwa  kwa ajiri ya kununua pembe jeo
 Pia masoko  ya  ununuzi wa zao hilo kufanyika kwa muda mrefu  kunachangia  vyama  vya msingi  kuchelewa kumaliza madeni yao kwenye  mabeki  na kusababisha  riba  kuongezeka  na  kuongeza  mzigo  kwa wakulima  
Katiba hotuba yake  Waziri wa kilimo Mwandisi   C ristopher Chiza  iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Paza  Mwamlima aliwataka wakulima wa Tumbaku  kuacha tabia ya kuchukua mikopo mikubwa ambayo hailingani na kilimo chao hivyo aliwashauri  wakulima wachukuwe mikopo kulingana na kilimo wanacholima
Alisema wakulima wa Tumbaku wajitahidi kuongeza uzalishaji  kwa kuongeza juhudi katika kilimo hicho  ili uzalishaji uzidi  kuongezeka
Alisema vyama vya ushirika vya msingi  vihakikishe vinakuwa na utaratibu wa kufunga hesabu zao kwa wakati  na wawasomee wakulima taarifa hizo za mapato na matumizi
 Chama kikuu cha ushirika wa wakulima wa Tumbaku cha Mkoa wa Katavi kinaundwa na vyama vya msingi vya Nsimbo, Katumba , Mpanda kati ,Ilunde , Ukonongo na Mishamo

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa