Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Wakulima wa Tumbaku wa Mkoa wa Katavi
wameuza zaidi ya kilo milioni 12.5
za Tumbaku zenye
thamani ya Dola za
Kimarekani milioni 28,748,210 katika msimu wa kilimi wa mwaka 2013 na 2014
Haya
yalielezwa katika Risara ya wakulima wa Tumbaku iliyosomwa na meneja Mkuu wa
wa chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Tumbaku cha Mkoa wa Katavi
LATCU Pius Kilo wakati
wa maadhimisho ya sherehe ya kutimiza miaka 20 ya chama kikuu hicho
yaliyofanyika kwenye viwanja vya Idara ya Mjini Mpanda
Mgeni Rasmi
kwenye maadhimisho hayo alikuwa ni Waziri wa
kilimo na ushirika mwandisi Cristopher Chiza ambae
aliwakilishwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi Paza Mwamlima
Kilo alisema msimu wa kilimo wa mwaka 2013 na 2014 wakulima wa Tumbaku wa Mkoa wa Katavi wameweza kuuza kilo 12,577,306 za Tumbaku zenye
thamani ya Dola za kimarekani milioni
28,748,,210 ambapo mkopo
wa pembejeo ulikuwa
wa thamani ya Dola 11,485,068 hivyo baada ya kulipa deni
wakulima walipata kiasi cha dola
17, 263, 148 kwa hela za
kitanzania ni sawa na shilingi Bilioni
27,621,028, 600 wastani kilo moja ilinunuliwa kwa bei ya tsh 1,600
Kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2014 na 2015
wakulima wanatarajia kulima hekta 14,006
ambazo zinatarajia kuzalisha kilo
15,343,420 za Tumbaku ambazo kwa
wastani wa msimu huu wa dola mbili
kwa kilo zinatarajiwa
zitapatikana dola za Kimarekani
30,686,840 sawa na Tsh shilingi Bilioni 49,098,944,000
Alisema uzalishaji wa Tumbaku kwa msimu huu
unatarajiwa kuongezeka kutokana na wingi wa wakulima ubora wa zao hilo na bei
kuwa nzuri ndio inafanya
kuwepo na ongezeko la uzalishaji
wa Tumbaku katika Mkoa wa Katavi
Alitaja baadhi ya
changamoto zinazowakabili wakulima wa Tumbaku kuwa ni uchache wa makampuni yanayo nunua
Tumbaku kuwa ni yaleyale ya miaka yote wakati uzalishaji wa
Tumbaku imeongezeka na wakati huo
makampuni yanayo nunua Tumbaku
yameanza kupunguza kasi
ya kununua Tumbaku
Changamoto
nyingine ni sheria ya kusajiri wa kulima wa kujitegemea na kuanzishwa
kwa Association katika maeneo yenye vyama vya ushirika
hari ambayo inasafanya kuwepo
kwa ulanguzi na utoroshwaji wa
Tumbaku hivyo husababisha vyama kushindwa kulipa madeni kwenye taasisi za kifedha
zilizowakopesha kwa kwa ajiri ya
kununua pembe jeo
Pia masoko
ya ununuzi wa zao hilo kufanyika
kwa muda mrefu kunachangia vyama
vya msingi kuchelewa kumaliza madeni
yao kwenye mabeki na kusababisha riba
kuongezeka na kuongeza
mzigo kwa wakulima
Katiba hotuba
yake Waziri wa kilimo Mwandisi C ristopher Chiza iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Paza Mwamlima aliwataka wakulima wa Tumbaku kuacha tabia ya kuchukua mikopo mikubwa
ambayo hailingani na kilimo chao hivyo aliwashauri wakulima wachukuwe mikopo kulingana na kilimo
wanacholima
Alisema wakulima
wa Tumbaku wajitahidi kuongeza uzalishaji
kwa kuongeza juhudi katika kilimo hicho ili uzalishaji uzidi kuongezeka
Alisema vyama vya
ushirika vya msingi vihakikishe vinakuwa
na utaratibu wa kufunga hesabu zao kwa wakati
na wawasomee wakulima taarifa hizo za mapato na matumizi
Chama kikuu cha ushirika wa wakulima wa
Tumbaku cha Mkoa wa Katavi kinaundwa na vyama vya msingi vya Nsimbo, Katumba ,
Mpanda kati ,Ilunde , Ukonongo na Mishamo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment