Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Wakulima wa vyama vya ushirika
k vya Msingi vya wakulima wa Tumbaku wa Mkoa wa Katavi wamepanda
jumla ya miti 4,247,748 sawa
na Hekta 1,699 katika msimu wa mwaka 2013 na 2014 kwa ajiri ya utunzaji
wa mazingira
Hayo yalielezwa hapo jana katika
risara ya wakulima wa Tumbaku wa
Mkoa wa Katavi iliyosomwa na Meneja mkuu
wa Chama kikuu cha wakulima wa Tumbaku
cha Mkoa wa Katavi (LATCU LTD)
wakati wa maadhimisho ya sherehe ya kutimiza miaka 20 ya Chama kikuu cha
wakulima wa Tumbaku LATCU LTD
yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya idara ya maji mjini Mpanda
Mgeni Rasmi
kwenye maadhimisho hayo alikuwa ni waziri wa kilimo chakula na ushirika Mwandisi C ristopher
Chiza ambae aliwakilishwa na kaimu mkuu
wa Mkoa wa Katavi Paza Mwamlima
Alisema
katika kuhakikisha kuwa kilimo cha Tumbaku
kinakuwa endelevu wakulima wa
tumbaku wa Mkoa wa Katavi swala
la utunzaji wa mazingira wamelipa
kipau
mbele kwa kupanda miti na kutunaza miti ya asili
Risala hiyo ilieleza kuwa vyama vya ushika vya msingi vya
wakulima wa Tumbaku vya Mkoa wa
Katavi vinatekeleza sheria na
kanuni za kilimo cha tumbaku zinaeleza kuwa kila mkulima wa tumbaku hapa
nchini anatakiwa kupanda
miti 550 na wakulima wa Tumbaku wa Mkoa
wa Katavi wanafanya hivyo
Kwa msimu wa mwaka 2014 na 2015 vyama vya ushirika vya msingi vya wakulima wa tumbaku vya
Mkoa wa Katavi vimeweka mkakati
wa wakulima kupanda jumla ya
miti 2,675,669 sawa na hekta 1,070 sambamba na kutenga
maeneo ya kuhifadhi miti
asili hekta 1,597 sawa na miti 3,993,631 ambazo zitatunzwa na kuifadhiwa
kwenye vyama vya msingi kwa ajiri
ya matumizi ya baadae
Kilo alisema
pamoja na juhudi hizo za vyama vya msingi vya ushirika kupambana na uharibi wa mazingira kwa kupanda
miti na kutenga maeneo
ya kuhifadhi na kutunza miti asili
wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali
Changamoto hizo alizitaja kuwa ni watu kuchoma moto ovyo na wachungaji wa mifugo kuchungia mifugo katika
mashamba ya miti na hifadhi
za miti ya asili
Hivyo
wanaiomba Serikali kuu na Serikali za
mitaa kuwa na sheria kali ili
kukabiliana na uharibufu huo
ambao unaweza ukasababisha vyama vya
ushirika na wakulima wao kukata tamaa
Kwa upande wake
Waziri wa kilimo chakula na ushirika
mwandisi Cristopher Chiza aliwataka wakulima wa Tumbaku hapa nchini kuangalia njia mbadala ya kutumia
makaa ya mawe kwa ajiri ya kuchomea tumbaku
badala ya kuendelea kutumia kuni
ili kuepukana na uharibifu wa mazingira
Alisema
viongozi wa ushirika wamekuwa ni
waoga kufanyiwa ukaguzi kwenye vyama
vyao kutokana na ubadilifu wanao kuwa
wameufanya kwenye vyama vyao
Hivyo aliwataka
wawe tayari kukaguliwa na wakaguzi kwani
vyama vingi vya ushirika vinashindwa kuendelea na hatimae kufa kutokana na
ubadliifu
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment