Home » » WANAFUNZI WAWALILIA WAALIMU WAO KUTEMBEA UMBALI WA KILOMETA NNE KUTAFUTA MAJI

WANAFUNZI WAWALILIA WAALIMU WAO KUTEMBEA UMBALI WA KILOMETA NNE KUTAFUTA MAJI


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kabulonge iliyoko katika makazi ya Wakimbizi ya Katumba Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi  wamelalamikia shida wanayo pata waalimu wao ya kutembea umbali wa kilometa nne kwa ajiri ya kutafuta huduma ya maji  kutokana   na shule hiyo kutokuwa na huduma ya maji
Kilio hicho cha wanafunzi wa Shule hiyo kilitolewa hapo jana kwenye  risarayao walioisoma mbele ya mgeni rasmi mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wakulima wenyeviwanda wakulima na wafugaji wa Mkoa wa Katavi Hassanal Shabir Dala wakati wa mahafari 32  ya darasa la saba yalifanyika shuleni hapo
Katika risala hiyo ilisomwa na mwanafunzi Odilia  Eliazek walieleza kuwa  shule hiyo ya  Kabulonge i ilianzishwa toka mwaka 1974 lakini  haijawahi kuwa na huduma ya maji shuleni hapo
 Walisema toka shule hiyo ilipo anzishwa  imekuwa  haina huduma ya maji hari inayosababisha waalimu wao kutembea umbali wa kilometa  nne kwenda kijiji cha jirani kutafuta huduma ya maji hivyo waliiomba Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo iwachimbie kisima cha maji ili waweze kuondokana na tatizo hilo
  Pia walieleza  wapo baadhi ya wazazi  wamekuwa na tabia ya kuwatelekeza watoto wao wanaokuwa  wamefaulu kujiunga na masomo ya Sekondari  kwa kushindwa kwa makusudi  kuwalipia ada za shule watoto wao na kuwananulia  vifaa vya shuleni
Nae  mgeni rasmi wa mahafari hayo  Hassanal Shabil Dala aliwataka wazazi wa wanafunzi hao waakikishe  wanafunzi wanakao faulu kujiunga na kidato cha kwanza hapo mwakani  wanawapeleka shule  na ambao watakuwa hawakufaulu  wawatafutie shule
Alisema wazazi wanao wajibu wakuwalea watoto wao  vizuri  iliwanapomaliza   elimu ya msingi  waweze  kuendelea na masomo zaidi badala ya  kuwaacha   wazurule  mitaani
 Dala aliwaasa   wanafunzi hao wasiwe na tabia  ya kukimbilia mitaani na kucheza madisko  ambayo hayana  umuhimu wowote kwenye maisha yao  wala manufaa
 Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Litabunga Godfrey Lusambo  alisema atajitahidi  kumshauri   mkurugenzi wa Halmashauri ya Nsimbo kupeleka  mradi wa maji kwenye shule hiyo
Alisema  shule hizo za msingi ambazo zipo kwenye makazi  ya wakimbizi  ya Katumba  zilikuwa zinamilikiwa na  na  shirika  la kuwaudumia wakimbizi TCRS  lakini  hivi karibuni ndio ziwemekabidhiwa kwa Halmashauri ya Nsimbo
 Mwalimu Mkuu wa shule hiyo   Elius  Nguard  alimshukuru  Hassanal  Dala kwa  kuipatia msaada wa sola ya umeme ambayo  itawasaidia kendelea na  kuwafundisha masomo wanafunzi  mida ya usiku
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa