Home » » MKOA WA KATAVI WAJIWEKEA MALENGO YA KUZALISHA TANI 892,844 ZA MAZAO YA NAFAKA IFIKIAPO MWAKA 2018

MKOA WA KATAVI WAJIWEKEA MALENGO YA KUZALISHA TANI 892,844 ZA MAZAO YA NAFAKA IFIKIAPO MWAKA 2018



Na  Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi
 Mkoa wa Katavi  katika kuhakikisha  unakuwa na  chakula cha kutosha  na kuuza  mazao  nje ya Mkoa  umejiwekea  malengo  ya kuongeza  uzalishaji  wa mazao  ya chakula   kutoka tani  696 404  za mwaka 2013   hadi kufikia  tani  892,844 ifikiapo mwaka 2018
Hayo yalisemwa hapo juzi na Mkuu wa Mkoa wa Katavi DR Rajab Rutengwe wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Katavi kwenye uwanja wa shule ya Msingi Kashaulili mjini Mpanda wakati alipokuwa  akifungua maazimisho ya sherehe  za siku ya chakula Duniani  zinazoazimishwa kitaifa Mkoani Katavi  ambapo kilele cha sherehe hizo zitakuwa oktoba 16
Mkuu huyo wa Mkoa aliwaeleza  msimu wa kilimo mwa mwaka 2013 na 2014 Mkoa wa Katavi  ulizalisha tani  za mahindi  289,413 na mpunga zilizalishwa  tani 289,413
 Alifafanua Mkoa  wa Katavi  umejiwekea  malengo  ya  kuongeza  uzalishaji  wa mazao ya chakula  kutoka tani  448,201 za mwaka 2013 hadi kufikia tani 892’ 844 ifikiapo mwaka  2018 na mazao  ya mizizi  na ndizi  kutoka  tani 609,078 za mwaka 2013 hadi kufikia tani 880.155 ifikiapo  mwaka 2018
Alisema  uzalishaji wa mazao  ya mafuta  karanga  ufuta  na alizeti  kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2013 na 2014 ulikuwa  ni tani  87,535 na itakapo fikia mwaka 2018 uzalishaji utakuwa ni tani 298.155
 Dr Rutengwe aliwataka wananchi wa Mkoa wa Katavi kutumia maadhimisho hayo ya siku ya chakula Duniani  kwa kujifunza mbinu mbalimbali  za kuendeleza  sekta ya kilimo
Pia watumie furusa hiyo kwa kuuliza  yale  yanawatatiza  kwani  wataalamu  ,watafiti wakulima na wafugaji  waliofika kwenye maadhimisho hayo  kutoka  pande  mbalimbali  za Nchi  watawasaidia  kuwapatia ufumbuzi  wa changamoto zao
 Alisema kwa upande wa sekta ya  mifugo  Mkoa wa Katavi umelenga  kuboresha  mifugo  na mazao yatokanayo na mifugo kwa  kuboresha na kuongeza  usindikaji  na thamani  za  bidhaa za mazao ya mifugo  kuongeza  mazao ya uvuvi  na kuongeza uzalishaji  wa mazao ya nyuki
Alifafanua yote hayo yameainishwa  katika  mpango  wa kuendeleza  kilimo  Mkoani Katavi (KADEP) ambao  utazindiliwa  rasmi hivi  karibuni
 Mkoa  kupitia  Halmashauri zake  zote  umehimiza  suala la ufugaji  wa nyuki  kama njia moja wapo  ya kujipatia  kipato  na kuondokana na umasikini  kwa wananchi alisema Mkuu huyo wa Mkoa wa Katavi
DR Rajab Rutengwe  alieleza  Mkoa wa Katavi  una jumla ya wafugaji wa nyuki  wapatao 8,516 katika msimu  wa mwaka 2013 mazao ya nyuki yameongezeka  kutoka tani  556 za asali  za mwaka 2012 na kufikia  tani  788 na uzalishaji wa nta  umeongezeka  kutoka tani 300 hadi kufikia  tani 325
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi msaidizi   wa Wizara ya kilimo na ushirika  wa kitengo cha  idara ya usala wa chakula Josephin Amolo alieleza kuwa maadhimisho hayo ya siku ya chakula Duniani yalianzishwa mwaka  1981 na mwaka huu yatakuwa ni maadhimisho ya 34
Alisema kilimo cha Nchi ya Tanzania  kwa sehemu kubwa kinaendeshwa na wakulima wadogo  hivyo ili kiweze kuendelea  lazima kiende sambamba  na utunzaji wa mazingira

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa