Home » » TEKINONOLOJIA DUNI NDIO SABABU INAYOKWAMISHA KILIMO KISIKUWE IPASAVYO KATAVI

TEKINONOLOJIA DUNI NDIO SABABU INAYOKWAMISHA KILIMO KISIKUWE IPASAVYO KATAVI



Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Moja ya sababu  inayosababisha  kilimo  kisikue  ipasavyo  Mkoani imeelezwa kuwa  ni pamoja na sababu  ya wakulima wengi  kuendelea  kutumia Teknolojia  duni kwa wakulima  kuendelea kulima  mazao  yao kwa  kutumia jembe la mkono   
Hayo  yalisemwa hapo juzi na Mkuu wa Mkoa wa Katavi DR Rajab Rutengwe wakati alipokuwa akihutubia kwenye  mkutano wa hadhara uliofanyika  kwenye uwanja wa shule ya msingi Kashaulili mjini Mpanda  alipokuwa akifungua maadhimisho ya siku ya chakula Duniani yanayofanyika Kitaifa Mkoani Katavi
Alisema kuwa baadhi ya wakulima kuendelea  kutegemea jembe la mkono kwenye kilimo chao  kumesababisha  washindwe kupanua  maeneo yao  wanayolima mazao  mbalimbali
 Pia   wakulima kuendelea kutumia jembe la mkono  huwafanya watumie muda mwingi  mashambani   kutokana na kutegemea jrmbe la mkono  na kupelekea  vijana  kuichukia  kazi ya kilimo  na kuiacha ifanywe na  wazee peke yao
DR Rutengwe alifafanua kuwa  matumizi ya kilimo cha  kutumia  matrekta katika kilimo  Mkoani Katavi ni asilimia tano  wanyama kazi ni asilimia  kumi na tano  na jembe la mkono ni asilimia themanini  hari hiyo inaonyesha  wazi kuwa mkoa wa Katavi  bado upo nyuma  katika matumizi sahihi  ya tekinolojia
Alifafanua  ilikufikia lengo  la uzalishaji  wa chakula cha kutosha  kwenye ngazi ya kaya  na kuboresha  kilimo Serikali  imekuwa ikitowa  ruzuku  katika mbolea na mbegu bora  kwa njia  ya ruzuku  ya pembejeo  wakulima wengi  wameweza  kuongeza uzalishaji  wa mazao ya mahindi na mpunga
Alieleza  kwa msimu  huu wa kilimo wa mwaka 2013 na 2014  Serikali itatoa  pembejeo  kupitia vikundi  na vyama vya ushirika  ambapo wakulima waliopo katika  vikundi watawezeshwa  kukopa  kwenye mabenki  na kununua pembejeo kulingana mahitaji yao
 Alitowa wito  kwa wananchi  wote kujiunga  katika vikundi  na  kujisajili  katika taratibu  zinazotakiwa  ili waweze  kukopesheka
Mkuu huyo wa Mkoa alisema  mkoa umejiwekea lengo  la kuongezaeneo la uzalishaji  wa mazao  ya chakula  kupitia kilimo cha umwagiliaji  mashambani  kutoka hekta   21,336 za mwaka 2012na 2013 hadi  kufikia hekta  25,774 ifikiapo mwaka 2018 malengo hayo yatafikiwa kupitia BRN kwa kuboresha  skimu saba  za mwagiliji  zilizopo Mkoani Katavi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa