Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mkoa wa Katavi
katika kuhakikisha unakuwa
na chakula cha kutosha na kuuza mazao nje ya Mkoa
umejiwekea malengo ya kuongeza
uzalishaji wa mazao ya chakula
kutoka tani 696 404 za mwaka 2013
hadi kufikia tani 892,844 ifikiapo mwaka 2018
Hayo yalisemwa
hapo juzi na Mkuu wa Mkoa wa Katavi DR Rajab Rutengwe wakati alipokuwa akiwahutubia
wananchi wa Mkoa wa Katavi kwenye uwanja wa shule ya Msingi Kashaulili mjini
Mpanda wakati alipokuwa akifungua
maazimisho ya sherehe za siku ya chakula
Duniani zinazoazimishwa kitaifa Mkoani
Katavi ambapo kilele cha sherehe hizo
zitakuwa oktoba 16
Mkuu huyo wa Mkoa
aliwaeleza msimu wa kilimo mwa mwaka
2013 na 2014 Mkoa wa Katavi ulizalisha
tani za mahindi 289,413 na mpunga zilizalishwa tani 289,413
Alifafanua Mkoa wa Katavi
umejiwekea malengo ya
kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula kutoka tani
448,201 za mwaka 2013 hadi kufikia tani 892’ 844 ifikiapo mwaka 2018 na mazao
ya mizizi na ndizi kutoka
tani 609,078 za mwaka 2013 hadi kufikia tani 880.155 ifikiapo mwaka 2018
Alisema uzalishaji wa mazao ya mafuta
karanga ufuta na alizeti
kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2013 na 2014 ulikuwa ni tani
87,535 na itakapo fikia mwaka 2018 uzalishaji utakuwa ni tani 298.155
Dr Rutengwe aliwataka wananchi wa Mkoa wa
Katavi kutumia maadhimisho hayo ya siku ya chakula Duniani kwa kujifunza mbinu mbalimbali za kuendeleza
sekta ya kilimo
Pia watumie
furusa hiyo kwa kuuliza yale yanawatatiza kwani
wataalamu ,watafiti wakulima na
wafugaji waliofika kwenye maadhimisho
hayo kutoka pande
mbalimbali za Nchi watawasaidia
kuwapatia ufumbuzi wa changamoto
zao
Alisema kwa upande wa sekta ya mifugo
Mkoa wa Katavi umelenga kuboresha mifugo
na mazao yatokanayo na mifugo kwa
kuboresha na kuongeza usindikaji na thamani
za bidhaa za mazao ya mifugo kuongeza
mazao ya uvuvi na kuongeza
uzalishaji wa mazao ya nyuki
Alifafanua yote
hayo yameainishwa katika mpango
wa kuendeleza kilimo Mkoani Katavi (KADEP) ambao utazindiliwa
rasmi hivi karibuni
Mkoa
kupitia Halmashauri zake zote
umehimiza suala la ufugaji wa nyuki
kama njia moja wapo ya kujipatia kipato
na kuondokana na umasikini kwa
wananchi alisema Mkuu huyo wa Mkoa wa Katavi
DR Rajab
Rutengwe alieleza Mkoa wa Katavi una jumla ya wafugaji wa nyuki wapatao 8,516 katika msimu wa mwaka 2013 mazao ya nyuki
yameongezeka kutoka tani 556 za asali
za mwaka 2012 na kufikia tani 788 na uzalishaji wa nta umeongezeka
kutoka tani 300 hadi kufikia tani
325
Kwa upande wake
Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya
kilimo na ushirika wa kitengo cha idara ya usala wa chakula Josephin Amolo
alieleza kuwa maadhimisho hayo ya siku ya chakula Duniani yalianzishwa
mwaka 1981 na mwaka huu yatakuwa ni
maadhimisho ya 34
Alisema kilimo
cha Nchi ya Tanzania kwa sehemu kubwa
kinaendeshwa na wakulima wadogo hivyo
ili kiweze kuendelea lazima kiende
sambamba na utunzaji wa mazingira
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment