Friday, October 17, 2014

HALMASHAURI WAHAMASISHENI WAKULIMA KUJENGA MAGHALA YA KUHIFADHIA MAZAO YAO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Halmashauri zalizopo katika Mkoa wa Katavi zimetakiwa kuwahamasisha wakulima wao kujenga maghala ya kuhifadhia mazao yao badala ya kuwahamasisha tuu waongeze kilimo  cha mazao mbalimbali
 Wito huo umetolewa hapo juzi  na kaimu Mkurugenzi wa  wizara ya kilimo na ushirika wa kitengo cha usala wa  chakula   Jesephin Amolo  kwenye shamba  la  Waziri Mkuu Mizengo Pinda  lilipo katika kijiji cha Kibaoni Wilayani Mlele  Mkoa wa Katavi  wakati akiwa na viongozi mbalimbali wa Wizara ya kilimo na ushirika  na Mifugo walipotembelea shamba hilo walipokuwa wakikagua miradi ya maendeleo kwenye maadhimisho ya siku ya chakula Duniani yanayofanyika kitaifa Mkoani hapa
 Alisema  Halmashauri zilizopo  katika Mkoa wa Katavi ziwasaidie wakulima kwa kuwahamasisha kujenga maghala ya kuhifadhi mazao  na    Halmashauri hizo  nazo pia zijiwekee utaratibu wa kujenga maghala  ya kutosha kwa ajili ya kuifadhia mazao ya wakulima
Alifafanua  wakulima  wengi wanapoteza mazao yao mengi yakiwa shambani  kutokana na kutokuwa na maghala ya  kuhifadhia mazao yao mbalimbali wanayokuwa wameyalima
 Josephin  alieleza  ni vizuri  wakulima watambue kuwa wanapo zalisha mazao yao ni lazima wajue  soko linataka nini  kwani wapo baadhi ya wakulima wanalima tuu lakini  mazao yao yamekosa soko kutokana na kutokuwa na ubora
 Alisema  wakulima  wanapo weka dawa ya kuuwa  wadudu  ni  vema wakazingatia  utaalamu  kwani  lazima wajue  chakula kinacholimwa lazima kiwe salama kwa watuaji
 Kwa upande wake afisa habari wa Wizara ya Kilimo na ushirika Dr  Richald Kasuga alieleza kuwa  wakulima  ni vizuri wakulima watambue kuwa wazao yao wanayozalisha   ni lazima yawe na ubora  vinginevyo  chakula hicho hakitakuwa  salama kwa watuaji
 Alisema mazao ya wakulima wa Tanzania yamekuwa yakikosa  soko  nje ya Nchi kutokana na mazao hayo  kukosa ubora kwenye masoko ya kimataifa
 Nae afisa ugani wa Kata ya Kibaoni aliwaeleza viongozi hao kuwa shamba hilo la waziri Mkuu Mizengo Pinda lina ukubwa wa Ekali mia mbili
Alisema msimu huu  zililimwa ekali 55 na Waziri Mkuu ameweza kuvuna jumla ya magunia 800 ya mahindi na msimu uliopita  alivuna magunia 700 ya mahindi
 Mwakilishi wa Afisa kilimo wa Mkoa wa Katavi  joanith Mkiwa  alieleza shamba hilo na Waziri Mkuu limekuwa likitumiwa na  wakulima wa Kata hiyo kwa kujifunzia kilimo chora na chakisasa
 Alisema kupitia shamba hilo la mfano wakulima wengi wameanza kunufaika kwani  wamefanikiwa  kuongeza uzalishaji wa mazao yao tofauti na hapo awali

No comments:

Post a Comment