Home » » MAKAMPUNI YA PEMBEJEO KATAVI WAAGIZWA KUWA NA MASHAMBA DARASA

MAKAMPUNI YA PEMBEJEO KATAVI WAAGIZWA KUWA NA MASHAMBA DARASA


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
Serikali    Mkoani  Katavi  imeyaagiza  makapuni  ya pembejeo za kilimo  ambayo  yatapewa   kibali  cha kuasambaza pembejeo za kilimo katika msimu huu wa kilimo  wa  mwaka 2014 na 2015 kuhakikisha wanakuwa na  shamba  darasa kwenvye  eneo watakalokuwa wanafanyia shughuli   vinginevyo hawatapata vibali vya kuwaruhusu  kufanya shughuli za  kusambaza pembejeo katika Mkoa wa Katavi
Kauli hiyo imetolewa hapo juzi na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr  Rajab Rutengwe wakati alipokuwa akizungumza   na waandishi wa habari ofisini  kwake jinsi  Mkoa wa Katavi  uliweka mikakati ya  kuboresha zaidi kilimo msimu huu
 Dr  Rutengwe  alisema  Mkoa wa Katavi umeamua kuchukua amuzi huo  ili kuweza  kubaini  ubora wa  pembejeo zitakazosambazwa na makampuni hayo ya pembejeo
 Lengo jingine la Mkoa ni kutaka  makapuni  hayo  kuyatumia mashamba yao darasa  kuwafundishia wakulima  namna ya kutumia mbegu za makampuni yao na mbolea  pamoja na madawa ya kuulia wadudu
 Alisema utaratibu huu utasaidia  kuweza kugundua mbegu  ambazo  zitakuwa  hazisitahili  kutumiwa na wakulima  kwa ajiri ya kilimo katika Mkoa wa Katavi
 Alifafanua  utaratibu  huo  utapunguza kwa kiasi kikubwa malalamiko ya wakulima  ya pindi mazao yao yatakapokuwa yamepandwa na kushindwa kuota
Alisema makampuni yote ya pembejeo  ambayo yameomba kusambaza pembejeo katika Mkoa wa Katavi yameisha  elezwa utaratibu huo  na wamekubali utaribu huo
Msimu wa kilimo wa mwaka jana kulikuwa na malalamiko katika baadhi ya maeneo mbalimbali  mkoani hapa   ambapo  wakulima  walilalamikia baadhi ya mbegu  walizosambaziwa zilishindwa kuota  na Mkoa  ulilazimika kuyaagiza makampuni  yaliosambaza mbegu kuwafidia mbegu nyingine wakulima  
 Alieleza kwa msimu huu tatizo hilo halitakuwepo kabisa kwa Mkoa huu  kwani mbegu atakazo uziwa mkulima ndizo  zitakazokuwa zimepandwa kwenye mashamba darasa ya  kampuni husika na kampuni yoyote itakayo bainika imesambaza pembejeo  zisizo na ubora itachukuliwa hatua za kisheria 

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa