Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Wakter
Mguluchuma
Katavi
Jumla ya watu
392,174 Mkoani Katavi wanatarajiwa
kupatiwa chanjo ya kujikinga na
uginjwa wa surua na Rubellana magonjwa ambayo
yalikuwa hayajapewa kipaumbele kwenye kampeni shirikishi ya chanjo ya Surua na Rubella
Hayo yalisemwa
hapo jana na mganga mkuu wa Mkoa wa Katavi DR
Yahaya Hussen wakati alipokuwa akitowa taarifa ya maandalizi ya kampeni shirikishi ya
chanjo ya surua na arubella na
magonjwa yasiyopewa kipaombele kwenye kikao cha kamati ya afya ya Mkoa wa
Katavi kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa Mkoa wa
Katavi
DR Yahaya alieleza kuwa kampeni hiyo imepangwa kuanza Oktaba 18 na kumalizika oktoba 24
itazindiliwa kesho na Mkuu wa Mkoa wa Katavi katika kijiji cha Nsimbo wilaya ya Mlele
Alisema kampeni hiyo imelenga pia
kudhibiti magonjwa ya matende ,mabusha , usubi na minyoo ya tumbo
ambapo watu wenye umri wa kuanzia miaka mitano na kuendelea watapatiwa dawa za
kutumia aina ya Albendazole
na ivermectin
Alifafanua chanjo ya surua na Rubella
itatolewa kwa watoto walio na umri wa
miezi tisa mpaka watoto wenye umri wa chini ya miaka 15
Kwa upande wake
mratibu wa chanjo wa Mkoa wa Katavi Stephano Kahindi alielaza
kuwaMkoa wa Katavi umeisha towa
mafunzo kwa timu ya za wataalamu wa afya katika Halmashauri zote za Mkoa huu
AidhaMkoa
umefanya usimamizi elekezi kwenye Halmashauri za Wilyaya Mpanda ,Nimbo ,
Mlele na Halmashauri ya Mji wa Mpanda
juu ya maandalizi ya kampeni shirikishi
ya surua na rubella
Nae mwakilishi wa shirika la afya ulimwenguni
(WHO) kwa mikoa
ya kanda za nyanda za juu
DR Bonifasi Makelemi alieleza
kuwa kuna uthibitisho kuwa kila
wilaya hapa nchini ina maambukizi ya magonjwa
ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele
Aliyataja
magonjwa hayo kuwa ni ukoma ,tauni ,kichaa cha mbwa ,matende ,mabusha kichocho ,usubi ,dengue , minyoo , homa ya
malale na homa ya ini
RD Malelemi alieleza inakadiriwa takribani
watu miliioni tano wameathirika
na magonjwa hayo nchini
Tanzania na kupelekea nguvu kazi ya
Taifa kupungua
0 comments:
Post a Comment