Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Serikali Mkoani
Katavi imeyaagiza makapuni
ya pembejeo za kilimo ambayo yatapewa
kibali cha kuasambaza pembejeo za
kilimo katika msimu huu wa kilimo wa mwaka 2014 na 2015 kuhakikisha wanakuwa
na shamba darasa kwenvye eneo watakalokuwa wanafanyia shughuli vinginevyo hawatapata vibali vya
kuwaruhusu kufanya shughuli za kusambaza pembejeo katika Mkoa wa Katavi
Kauli hiyo
imetolewa hapo juzi na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Rajab Rutengwe wakati alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake jinsi Mkoa wa Katavi uliweka mikakati ya kuboresha zaidi kilimo msimu huu
Dr
Rutengwe alisema Mkoa wa Katavi umeamua kuchukua amuzi
huo ili kuweza kubaini
ubora wa pembejeo
zitakazosambazwa na makampuni hayo ya pembejeo
Lengo jingine la Mkoa ni kutaka makapuni
hayo kuyatumia mashamba yao
darasa kuwafundishia wakulima namna ya kutumia mbegu za makampuni yao na
mbolea pamoja na madawa ya kuulia wadudu
Alisema utaratibu huu utasaidia kuweza kugundua mbegu ambazo
zitakuwa hazisitahili kutumiwa na wakulima kwa ajiri ya kilimo katika Mkoa wa Katavi
Alifafanua
utaratibu huo utapunguza kwa kiasi kikubwa malalamiko ya
wakulima ya pindi mazao yao yatakapokuwa
yamepandwa na kushindwa kuota
Alisema makampuni
yote ya pembejeo ambayo yameomba
kusambaza pembejeo katika Mkoa wa Katavi yameisha elezwa utaratibu huo na wamekubali utaribu huo
Msimu wa kilimo
wa mwaka jana kulikuwa na malalamiko katika baadhi ya maeneo mbalimbali mkoani hapa ambapo
wakulima walilalamikia baadhi ya
mbegu walizosambaziwa zilishindwa kuota na Mkoa
ulilazimika kuyaagiza makampuni
yaliosambaza mbegu kuwafidia mbegu nyingine wakulima
Alieleza kwa msimu huu tatizo hilo
halitakuwepo kabisa kwa Mkoa huu kwani
mbegu atakazo uziwa mkulima ndizo
zitakazokuwa zimepandwa kwenye mashamba darasa ya kampuni husika na kampuni yoyote itakayo
bainika imesambaza pembejeo zisizo na
ubora itachukuliwa hatua za kisheria
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
No comments:
Post a Comment