Home » » HALMASHAURI YA NSIMBO YAKUSANYA ZAIDI YA TSH MILIONI 400 KWA KIPINDI CHA MWEZI MMOJA

HALMASHAURI YA NSIMBO YAKUSANYA ZAIDI YA TSH MILIONI 400 KWA KIPINDI CHA MWEZI MMOJA


Na  Walter  Mguluchuma
Katavi
 Halimashauri ya Nsimbo  katika Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi imekusanya mapato  ya ndani  zaidi ya shilingi milioni  400 katika kapindi i  cha mwezi mmoja  ikiwa ni sawa  asalimia 91.2l la lengo la kukusanya  kwa mwezi Ts milioni 451
Hayo yalisemwa hap jana na mwenyekiti wa Halimashauri ya  Nsimbo  Mohamed Asenga wakati  akitowa  taarifa ya kamati ya fedha uchumi na mipango  mbele  ya  kikao cha Baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo kilichofanyika  kwenye ofisi ya Halmashauri  ya Nsimbo  
Alilieleza baraza hilo  kwa kipindi cha mwezi june  mwaka huu  Halimashauri  kukusanya  imeweza kiasi cha shilingi  milioni 411,769,611 ikiwa  ni sawa na 91.2 ya lengo kwa mwezi huu la kukusanya kiasi cha shilingi milioni 451,507,275
Alisema mapato hayo yametokana na vyanzo mbalimbali  vya mapato ya ndani  ya Halmashauri hiyo iliyoanzishwa hivi karibuni
Asenga alilieleza baraza hilo la madiwani  kuwa kwa kipindi cha mwaka  julai  2013 hadi june 2014 Halimashaur ya Nsimbo  ilikusanya kiasi cha shilingi milioni  753,042,184 sawa na asilimia 105.6 la lengo la kukusanya mapato  kwa mwaka shilingi milioni  713,328,000 kwa mapato ya ndani
 Alisema  Halimashauri  ya Nsimbo  katika maandalizi yake ya kuifanya Halimashauri hiyo kuwa Halimashauri ya Mji mdogo imetumia kiasi cha shilingi milioni 250 kwa ajiri ya pimaji wa viwanja 965 na uchoraji wa ramani
Nae diwani wa Kata ya Magamba aliiomba Halimashauri hiyo  kuwchukulia hatua watendaji wote wa Vijiji ambao  wamekuwa na tabia ya kutowasomea wananchi  mapato na matumizi kwenye vijiji vyao
 Alisema kwani watendaji hao  wamesababisha  wananchi wengi  vijijini  ambao walikuwa na moyo wa  kuchangia  michango ya maendeleo  kuvunjika moyo na kucha kuchangia michango
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa