Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Katavi
Halmashauri
zalizopo katika Mkoa wa Katavi zimetakiwa kuwahamasisha wakulima wao kujenga
maghala ya kuhifadhia mazao yao badala ya kuwahamasisha tuu waongeze
kilimo cha mazao mbalimbali
Wito huo umetolewa hapo juzi na kaimu Mkurugenzi wa wizara ya kilimo na ushirika wa kitengo cha
usala wa chakula Jesephin Amolo kwenye shamba
la Waziri Mkuu Mizengo Pinda lilipo katika kijiji cha Kibaoni Wilayani
Mlele Mkoa wa Katavi wakati akiwa na viongozi mbalimbali wa Wizara
ya kilimo na ushirika na Mifugo
walipotembelea shamba hilo walipokuwa wakikagua miradi ya maendeleo kwenye
maadhimisho ya siku ya chakula Duniani yanayofanyika kitaifa Mkoani hapa
Alisema
Halmashauri zilizopo katika Mkoa
wa Katavi ziwasaidie wakulima kwa kuwahamasisha kujenga maghala ya kuhifadhi
mazao na Halmashauri hizo nazo pia zijiwekee utaratibu wa kujenga
maghala ya kutosha kwa ajili ya kuifadhia
mazao ya wakulima
Alifafanua wakulima
wengi wanapoteza mazao yao mengi yakiwa shambani kutokana na kutokuwa na maghala ya kuhifadhia mazao yao mbalimbali wanayokuwa
wameyalima
Josephin
alieleza ni vizuri wakulima watambue kuwa wanapo zalisha mazao
yao ni lazima wajue soko linataka
nini kwani wapo baadhi ya wakulima
wanalima tuu lakini mazao yao yamekosa
soko kutokana na kutokuwa na ubora
Alisema
wakulima wanapo weka dawa ya
kuuwa wadudu ni
vema wakazingatia utaalamu kwani
lazima wajue chakula kinacholimwa
lazima kiwe salama kwa watuaji
Kwa upande wake afisa habari wa Wizara ya
Kilimo na ushirika Dr Richald Kasuga
alieleza kuwa wakulima ni vizuri wakulima watambue kuwa wazao yao
wanayozalisha ni lazima yawe na
ubora vinginevyo chakula hicho hakitakuwa salama kwa watuaji
Alisema mazao ya wakulima wa Tanzania yamekuwa
yakikosa soko nje ya Nchi kutokana na mazao hayo kukosa ubora kwenye masoko ya kimataifa
Nae afisa ugani wa Kata ya Kibaoni aliwaeleza
viongozi hao kuwa shamba hilo la waziri Mkuu Mizengo Pinda lina ukubwa wa Ekali
mia mbili
Alisema msimu
huu zililimwa ekali 55 na Waziri Mkuu
ameweza kuvuna jumla ya magunia 800 ya mahindi na msimu uliopita alivuna magunia 700 ya mahindi
Mwakilishi wa Afisa kilimo wa Mkoa wa
Katavi joanith Mkiwa alieleza shamba hilo na Waziri Mkuu limekuwa
likitumiwa na wakulima wa Kata hiyo kwa
kujifunzia kilimo chora na chakisasa
Alisema kupitia shamba hilo la mfano wakulima
wengi wameanza kunufaika kwani
wamefanikiwa kuongeza uzalishaji
wa mazao yao tofauti na hapo awali
0 comments:
Post a Comment