Home » » WANAKIJIJI WATISHIA KUTOMCHAGUA DIWANI ENDAPO HAWATA TENGENEZEWA BARABARA

WANAKIJIJI WATISHIA KUTOMCHAGUA DIWANI ENDAPO HAWATA TENGENEZEWA BARABARA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

  Na  Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi
 Wananchi wa Kijiji  cha Mwese Tarafa ya Mwese Wilaya ya Mpanda Mkoani   Katavi wametishia  kutomchagua  Diwani wa Kata yao  Juma  Hawazi kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwakani endapo hawatakuwa wametengenezewa barabara
 Hayo yalielezwa hivi    kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri Ya Wilaya ya Mpanda kilichofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya maji  mjini  Mpanda
Diwani wa viti maalumu wa Tarafa hiyo ya Mwese Thiodela Kisesa  alilieleza Baraza hilo la madiwani kuwa hivi karibuni walifanya mkutano wa hadhara  kwenye  Kijiji cha Mwese ayeye akiwa na Diwani Juma Hawazi na walipata wakati mgumu  kwenye mkutano huo
Diwani Kisesa  alieleza  wananchi hao walisema kwenyemkutano huo  kuwa hawata kuwa tayari kumchagua Diwani Hawazi  kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwakani endapo  barabara  ya kutoka kwenye kijiji hicho kuelekea kijiji wanachopakana nacho cha Kalya  kilichopo  Mkoani Kigoma endapo  haitakuwa imetengenezwa
Alifafanua  barabara hiyo ni ya muhimu sana kwa wananchi wa kijiji hicho kwani ndio inayo waunganisha wananchi wa vijiji hivyo viwili
 Alisema ilikumusuru  Diwani huyo kwenye uchaguzi mkuu wa ujao kwa wapiga kura wake Halmashauri ya Wilaya iangalie  uwezekano wa kuitengeneza barabara hiyo  
 Alieleza  matengenezo ya barabara hiyo  siyo lazima  yasubili fedha za kutoka kwa wafadhiri  bali Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  iangalie  uwezekano wa kutengeneza barabara hiyo kwa kutumia frdha za makusanyo  ya mapato yake ya ndani

Kwa upande wake Afisa  maendeleo na ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda  Jastine Tibenderana alisema Halmashauri hiyo ipo kwenye mpango wa kutengeneza barabara hiyo na inaendelea na mipango ya kupata wafadhili

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa