Home » » MWANAMKE AUWAWA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI NA MUME WAKE

MWANAMKE AUWAWA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI NA MUME WAKE



Na Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi
 Mtu mmoja aitwaye  Benadeta Bwetel (38) Mkazi wa Kijiji cha Uruwila  Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi  ameuwawa kikatili kwa kwa kupingwa na kitu kizito  kichwani na mume wake  aitwaye  Mohamed  Katyukuru   na kisha kufungiwa ndani ya nyumba
Kwa mujibu wa kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi kamishina msaidizi mwandamizi Dhahiri Kidavashari tukio hilolilitokea hapo Septemba 14 mwaka huu majira saa moja na nusu usiku asubuhi huko katika Kijiji cha Uruwila
 Alisema kabla ya  kifo hicho  marehemu  enzi za uhai wake  walikuwa wakiishi  pamoja na mume wake  Mohamedi  Katyukuru    pamoja na watoto wao wawili  Saidi Mohamedi (14) na Amuni  Mohamedi (11)
Katika maisha yao ya ndoa  waliokuwa wakiishi  pamoja  mume wa marehemu alikuwa na mazoea ya kumpiga mara kwa mara mkewe
Kidavashari alifafanua siku hiyo ya tukio  Raphael  Antony akiwa na   Albert Mayamba  ambao walikuwa ni jirani zake na marehemu  walitoka kwenye miji yao  na kuelekea shambani  na walipita njia  ya jirani na nyumba ya marehemu walishitushwa  hari ya hapo ilvyokuwa  ni tofauti  ya kawaida  ya siku zote  ambapo huwa wanaaikuta familia hiyo ikiwa hapo nyumbani
Alieleza  jirani hao wa marehemu  walipotembea mbele kidogo kutoka kwenye nyumba ya marehemu  waliona miburuzo   ya baiskeli  ikiwaimetokea nyumbani kwa marehemu  na ndipo waliposhitushwa na hari hiyo ns kuhisi kunatatizo kwenye nyumba hiyo
Majirani hao waliamua kwenda kutowa taarifa  kwenye mwenyekiti wa kijiji  na mwenyekiti wa kijij aliamua kuongozana na majirani hao hadi kwa mtendaji wa Kata  aitwaye Didasi  Buyaga
 Kamanda Kidavashari alisema  kishamtendaji wa kata  aliongozana  nao  hadi  nyumbani kwa  marehemu  na walikuta mlango umefungwa kwa kamba  kama ishara ya kuonyesha ndani ya nyumba  hiyo  haina mtu ndani
 Alisema walipiga  hodi   lakini hawakuweza kujibiwa  ndipo walipoamua kuvunja mlango na kuingia ndani  na kukuta  mareheumu  akiwa amekufa  kwa kupigwa na kitu kizito kichwani  lakini hawaku mkuta mume wake wala watoto na mpaka sasa hawajulikani waliko
 Chanzo cha mauwaji hayo  bado hakijajulikana  kwani mume wa  maehemu na watoto  mpaka sasa hawajulikani wako wapi  na upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa