Home » » Hatari: Watu wanane wamekufa Hapo hapo kwa ajari ya fuso na 11 wajeruhiwa‏

Hatari: Watu wanane wamekufa Hapo hapo kwa ajari ya fuso na 11 wajeruhiwa‏


Na  Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi
 Watu  nane wamekufa hapo   baada ya  Roli aina ya FUSO  waliokuwa wakisafiri kupinduka na wengine kumi na moja kujeruhiwa na kulazwa  hospitalini  baada ya gari walilokuwa wakisafiria  kupinduka   katika eneo la mlima  Katete uliopo katika Kijiji cha Milumba   Kata ya Kibaoni Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
 Ajari hiyo  ambayoililihusisha  Roli aina ya Fuso  lenye namba za usajiri    T 234 AXK  lilikuwa likiendeshwa na  Jamali Mohamed(42) Mkazi  wa   Mbagala Dares salaam  ilitokea  hapo Jana majira ya saa kumi na moja asubuhi  katika eneo la mlima  Katete  barabara itokayo Kibaoni W Ilayani Mlele kuelekea  Sumbawanga Mkoani Rukwa
 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi aliwataja waliokufa kuwa ni  Peter Lusambo (24),Ngelela Shaulitanga (29),   John Pius(32) ,  Linus (30) aliyetambulika kwa jina moja   wote hao wakazi wa Kata ya Kibaoni Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
Kidavashari aliwataja waliokufa wengine kuwa ni  Makono  Kisumu (23) Elias Mussa(28) wakazi wa  wilaya ya Geita Mwanza  Ally (34)Mkazi wa Dares salaam ambae alikuwa utingo wa gari hilo na   Abasi (28) alitambulika kwa jina moja mkazi wa Mtaa wa Mpanda Hotel Wilayani Mpanda
 Kamanda Kidavashari aliwataja majeruhi wa ajari hiyo ambao ni  Kaswagula  Linusi  25  Peter Mkalala 30 Peter Lusambo  20 Castory Kaombwe  23 Nassor  Ramadhan  22 wakazi wa Kata ya Kibaoni Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
 Wengine ni Salim Hassan  42  mkazi wa Mwanza  Jamari  Mohamed 42 Salumu  Njomoke  22 wakazi wa Dares salaam  John  Chambaneje  32  Mkazi wa  Mtaa wa Mpanda Hoteli  mjini  Mpanda
 Kamanda Kidavashari alisema  chanzo cha ajari  hiyo  ilitokana na  gari hilo  kukatika Propela  shafuti  hari iliyo pelekea  gari kuacha njia na kupinduka
 Alisema majeruhi hao wote  wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda na wanaendelea kupatiwa  matibabu  na hari zao zinaendelea vizuri
 Kidavashari alieleza  Dreva wa gari hilo  lililopata ajari  amekamatwa  na anatarajiwa  kufikishwa  mahakamani  mara baada ya upelelezi kukamilika


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa