Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda katika Mkoa wa wa Katavi inatarajiwa kukamilisha ujenzi wa majengo yote ya maabara za shule zote za Sekondari zilizopo katika Halmashauri hiyo
Hayao yalielezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Yassin Kibiriti wakati alipokuwa akifungua kikao cha kwanza cha cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda cha mwaka wafedha wa2014 na 2015 kilichofanyika jana kwenye ukumbi wa Idara ya Maji
Kiberiti alilieleza Baraza hilo la Madiwani kuwa hari ya ujenzi wa maabara katika shule za Sekondari zilizopo kwenye Halmashauri hiyo ni yakulidhisha sana
Alisema yapo majengo ya maabara kwenye shule za Sekondaro tayari yameisha kamilika na mengine ambayo bado yako kwenye hatua za kumalizia
Alifafanua hadi kufikia Oktoba 15 mwaka huu ujenzi wa majengo yote ya maabara kwenye shule zote za Sekondari zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda yatakuwa tayari yamekamilika
Alisema tatizo la kujenga majengo ya maabara kwenye shule za Sekondari kwenye Halmashauri hiyo halikuwa kubwa kama ambavyo ilivyo kwenye Halmashauri nyingine za hapa Nchini
Alieleza Halmashauri hiyo imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa majengo hayo kutokana na ushirikiano wa wananchi na wataalamu wa Halmashauri hiyo
Mwisho
0 comments:
Post a Comment