Home » » MUUZAJI WA BANGI ANUSURIKA KWENDA JELA KWA MIAKA MIWILI

MUUZAJI WA BANGI ANUSURIKA KWENDA JELA KWA MIAKA MIWILI

 Walter Mguluchuma -Katavi yetu
 MUUZA JI wa dawa  za kulevya  aina ya bangi , Ferdinand Makundi (40)
amenusurika  kutumikka kifungo  cha miaka  miwili jela  baada kulipa
faini  ya Sh 100,000- kwa kosa la kukutwa  na  kilo mbili  za  dawa
hiyo .

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama  ya Wilaya  ya Nkasi , mkoani Rukwa ,
Ramadhani Rugemalira  alimuhukumu  mshtakiwa huyo  ambaye ni mkazi wa
kijiji cha Mkole  wilayani  humo   kutumikia miaka miwili jela  au
kulipa  faini ya Sh 100,000-  baada ya kukiri kosa lake  mbele ya
mahakama hiyo .

Hata  hivyo mahakama  hiyo ilimwachia  mshtakiwa  huyo  baada ya
kulipa faini  hiyo  mahamani hapo .

Mshtakiwa  huyo  alikiri  kosa lake  hilo  baada ya Mwendesha Mashtaka
, Mkaguzi Msaidizi , Hamimu Gwelo  kumsomea   jana makosa  yake  ya
awali .

Kwa mujibu  wa Gwelo , mshtakiwa huyo  ni mzoefu  kwa  sababu aliwahi
awali  kutiwa  hatiani  na mahakama  hiyo  kwa kosa  la  kukutwa na
dawa  ya kulevya aina ya bangi  pia aliweza  kulipa faini na kuachiwa
hivyo aliiomba  mahakama impatie  adhabu kali   kwa kuwa bado
hajajifunza .

Hati  za mashtaka  mahakamani hapo  zinaonesha kuwa mshtakiwa huyo
alitenda  kosa hilo Mei , 14 mwaka  huu saa saba mchana  akiwa
nyumbani kwake  kijijini Mkole .
Alipotakiwa  kujitetea , mshtakiwa  aliiomba mahakama  hiyo impunguzie
 adhabu  kwa kuwa  ana watoto  kumi na  mke  wanaomtegemea .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa