Home »
» MAUAJI: MWANAUME AMCHOMA VISU MPENZI WAKE MPAKA KUMUUA KISHA NA YEYE KUJICHOMA VISU TUMBONI HADI KUTOKA UTUMBO NJE.
MAUAJI: MWANAUME AMCHOMA VISU MPENZI WAKE MPAKA KUMUUA KISHA NA YEYE KUJICHOMA VISU TUMBONI HADI KUTOKA UTUMBO NJE.
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi yetu Blog
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Cecilia Clement (20) Mkazi wa Mtaa wa Majengo Wilaya ya Mpanda ameuwawa kwa kuchomwa visu katika maeneo ya tumboni kifuani na shingoni na mpenzi wake Denson Kanubo (23)Mkazi wa Mtaa huo ambae nae alijichoma vifu vitatu tumboni na utumbo wake kutoka nje
Kwa mijibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari tukio hilo lilitokea hapo june 29 mwaka huu majira ya saa tatu asubuhi
Marehemu na Denson walikuwa wakiishi kwenye nyumba moja ya dada yake aitwaye Priisca Alex ambapo Denson alikuwa ni mpangaji katika nyumba hiyo na walikuwa na mahusiano ya kimapenzi
Kamanda Kidavashari alisema hivi karibuni watu hao waliingia katika mtaruku baada ya dada wa marehemu kubaini mahusiano yao ya kimapenzi hivyo alitaka marehemu aachane na Denson
Alisema siku moja kabla ya tukio la mauwaji hayo kulikuwa na malumbano ya wapenzi hao wawili kupitia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi walitumiana mara 26
Katika ujumbe huo marehemu alikuwa akimtukana matusi ya nguoni na pia marehemu alikuwa akimhusisha Danson na biashara ya meno ya Tembo katika meseji zake na kwamba siku zake za kukamatwa zimekaribia
Kidavashari alieleza Ndenson alikasirishwa na kitendo hicho cha kutumiwa meseji aliamua kwenda kumwamsha dada yake na mareu na kumwelezea jinsi alivyotukanwa
Alisema siku ya tehehe 29 baada wapenzi hao kuwa wameamka waliendelea kutishiana kuchomana visu na ujumbe wa mwishi wa marehemu aliomwandikia Danson ulikuwa ni huu nanukuu POA TUU UNICHOME KISU NICHOME UNAOUWEZO WA KUNICHOMA KISU MIMI WEWE....
Wakati dada wa marehemu akiwaanaendelea na shughuli zake za usafi wa nyumba alisikia maarehemu akipiga kelele za kuomba msaada huku akilia nakufa nakufa niachie
Dada wa marehemu alijaribu kuingia ndani ya chumba na ndipo aliposhudia mdogo wake akiwa anachomwa visu na yeye mwenyewe alitishiwa kuchomwa visu endapo athubutu kuingia ndani ya chumba hicho
Ndipo alitoka nje na kwenda kuomba msaada kwa majirani ambao walifika na kukuta tayari Cecilia ameisha kufa kwa kumchoma visu nae akiwa amejichoma vifu tumboni haadi utumbo kutoka nje
Jeshi la polisi lilifika kwenye eneo hilo na kufanya jitihada za kuokoa maisha ya majeruhi huyo na kufanikiwa kumkimbiza kwa ajiri ya matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambako amelazwa na hari yake inaendelea vizuri kidogo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:
Post a Comment