Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi yetu
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la
Kitola Jeremia(45)Mkazi wa Kijiji cha Vikonge
Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi ameuwawa kwa kukatwa na
panga sehemu za kichwani ,mkononi na tumboni hadi utumbo
wake kutoka nje na watu wawili wasiofahamika kwa sura wla majina yao
Tukio hilo la
mauwaji ya kusikitisha lilitokea hapo
june 29 mwaka huu majira ya saa
mbili usiku nyumbani kwa marehemu ambae
alikuwa akiishi kijini hapo na familia yake
Kwa mujibu wa
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa nje ya nyumba yake akiwa na
mke wake aitwaye Yulitha
Stephano (34) pamoja na wasaidizi
wake wakazi watatu wakijiandaa kula mlo wa usiku
Wakati wakila chakula ilitokea pikipiki moja
ambayo ilikuwaimewabeba watu wawili
waliokuwa wamevaa makoti meusi walipofika walimsalimiaana marehemu
na kisha walimweleza kuwa wao wametokea kijiji cha Mishamo lakini
wanaishi Kijiji cha Kakese na wamefika
hapo kwa ajiri ya kutafuta eneo la kuchungia mifugo yao
Kamanda
Kidavashari alisema marehemu
aliwajibu kuwa maeneo
yanapatikana yanapatikana hivyo walale
ilikesho yake asubuhi ili
aweze kuwapeleka kwa mwenyeji
ambae anaweza kuwapatia eneo la kuchungia mifugo yao
Baada ya mazungumzo hayo wageni hao
waliomba wapatiwe chakula na sehemu ya kulala ambapo wageni hao walitimiziwa ombi hilo na walipewa
chakula na kisha waliandaliwa sehemu ya kulala
Kidavashari
alieleza wagani hao baada ya kuonyeshwa sehemu ya kulala baadaye
waliamka na kwenda kwenye nyumba ambayo
alikuwa amelele marehemu na mke wake
na kisha walivunja mlango na
kuingia ndani na kuanza kumashambulia marehemu kwa mapanga
Alifafanua ndipo
mkewe alipoona mume wake anashambuliwa kwa mapanga alianza kupiga mayowe ya
kuomba msaada kwa majirani hata hivyo wauwaji hao walianza kumshambulia na yeye na
kumjeruhi kichwani
Alisema hata
hivyo mke wa marehemu alifanikiwa
kukimbia na kwenda kwenye
nyumba iliyokuwa kuwa jirani waliokuwa wamelala wasaidizi
watatu wa kazi wa marehemu na
kuwaeleza kilichotokea
Wasaidizi hao wa
kazi waliamka na kuongozana na mke wa marehemu
ili kwenda kutoa msaada na
walipofika kwenye nyumba aliyokuwa amelala marehemu walipoingia ndani walikuta tayari ameishafariki na wauwaji wakiwa wameisha tokomea kusiko julikana na pikipiki yao
Kamanda
Kidavashari alisema katika tukio
hilo wauwaji hawakutambulika wala namba za pikipiki hazikuweza kukaririwa kutokana na wenyeji wao kutokuwa na mashaka
juu ya watu hao ambao muda wote walikuwa
wamevaa kofia ngumu kichwani mwao (Helmet)
Alieleza uchunguzi
wa awali unaonyesha chanzo cha
mauwaji hayo kimetokana na
kugombea mali kati ya marehemu na
familia ya mke wake mkubwa aitwaye Justina
Philipo kwani marehemu aliondoka
kwenye kijiji cha Kakesa na
kumwacho mke mkubwa na kuondoka na mke mdogo na kuhamisha mali zote zikiwemo Ng’ombe
na mashine ya kusaga
Jeshi la polisi
linamshikilia Justina Philipo na
mama yake mzazi Kitola Simon
kwa ajili ya mahojiano zaidi kuhusiana na
tukio hilo
Home »
» AFARIKI DUNIA KWA KUKATWA NA MAPANGA KICHWANI,MKONONI, NA KUTOLEWA UTUMBO NJE.

0 comments:
Post a Comment