Home » » BARAZA LA MADIWANI LAUNDA TIMU YA KUCHUNGUZA MATUMIZI YA FEDHA TSH MILIONI 100

BARAZA LA MADIWANI LAUNDA TIMU YA KUCHUNGUZA MATUMIZI YA FEDHA TSH MILIONI 100

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji wa Mpanda  limeunda  timu ya  madiwani watano  kwa ajiri ya kuchunguza  fedha  kiasi cha shilingi milioni mia moja za fedha za maendeleo   za msimu wa mwaka 2012 na 2013  zinazodaiwa  kutumika kwa matumizi ya mengine bila idhini ya madiwani
Kikao hicho  cha dharula  cha  Baraza la madiwani kilifanyika hapo juzi katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji huo  kilichoongozwa na makamu wa Halmashauri hiyo  Yusuph Ngasa
Baraza la madiwani  lililazimika kufanya kikao hicho cha dharula  kufutia   Halmashauri hiyo  kutakiwa kujibu hoja ya mkaguzi mkuu wa hesabu  za Serikali kuibaini  Halmashauri hiyo  kutumia zaidi ya shilingi milioni mia moja  fedha za miradi ya maendeleo  katika msimu wa fedha wa mwaka 2012 na 2013
Katika kikao hicho makamu mwenye kiti wa Halmashauri hiyo alilieleza baraza hilo la madiwani kamati ya  fedha uchumi na mipango  iliyokutana kwa muda wa siku mbili kupitia  tuhuma  za Halmashauri hiyo zilizotolewa  na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ilibaini kuwepo  kwa tatizo hilo la watumishi  wa Halmashauri hiyo kutumia fedha kinyume na utaratibu
Diwani wa Kata ya Ilembo  Wensilausi Kaputa  alitaka Baraza lipatiwe majina ya watumishi ambao walihusika na huhamisha  fedha hizo  za miradi ya maendeleo kwa matumizi wakati wakijua ni kinyume cha sheria
Alieleza  inatia shaka hata fedha hizo  unaweza ukakuta zilitumika kwa matumizi yao  binafsi hivyo  ni vizuri wakachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo kwani tatizo hilo sio jipya kwa Halmashauri hiyo
Mwenyekiti  wa kikao hicho Yusuph Ngasa  aliwaeleza madiwani hao  kuwa kikao hicho kwa mujibu wa taratibu wa  kazi za kiutumishi  alina mamlaka ya kumwajibishi aliye kuwa  Mkurugenzi wa Halmashauri kwa kipindi hicho Joseph Mchina ambae ndiye aliyeidhinisha  fedha hizo zitumike kwa matumizi mengine na kwasa  yeye yuko  manispaa ya Singida
Alisema wao wanao uwezo wa kuwachukuli hatua za kinidhamu  watumishi wengine wawili ambao wanatuhumiwa kuwahamisha fedha hizo kinyume na utaratibu ambao ni mchumi wa Halmashauri  Frednandi Filimbi na mweka hazina Juma Luhomwa
Baada ya maelezo hayo ya mwenyekiti wa  kikao hicho  wajumbe wa baraza la madiwani walifikia uamuzi wa  kuunda kamati ya madiwani watano  ambayo itafanya kazi ya kuchunguza matumizi ya fedha hizo  na itaanza kazi leo  na itaongozwa na makamu mwenyekiti wa  Halmashauri Yusuph Ngasa na itafanya kazi kwa muda wa siku 14
 N a  walikubaliana  watumishi haowawili  wapewe  adhabu za kiutumishi za kukiuka  utaratibu wa kutumia  fedha za miradi ya maendeleo kwa matumizi mengine na kusababisha  miradi kushindwa kukamilika  kwani kosa hilo la kuhamisha fedha halihitaji kusubilia timu ya iliyoundwa  kitakacho subiliwa ni fedha wamezitumiaje
Aidha kwa Mkurugenzi Mchina walipendekezaKatibu Tawala wa Mkoa wa Katavi amwandikie katibu mkuu wa Tamisemi barua  kuhusu
 malalamiko ya  madiwani  jinsi Mkurugenzi huyo alivyohamisha fedha za miradi ya maendeleo kwa matumizi mengine bila idhini ya m

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa