Home » » AFARIKI DUNIA KWA KUKATWA NA MAPANGA KICHWANI,MKONONI, NA KUTOLEWA UTUMBO NJE.

AFARIKI DUNIA KWA KUKATWA NA MAPANGA KICHWANI,MKONONI, NA KUTOLEWA UTUMBO NJE.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na  Walter  Mguluchuma
Mpanda Katavi yetu
 Mtu mmoja aliyejulikana  kwa jina la  Kitola  Jeremia(45)Mkazi wa Kijiji  cha Vikonge  Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi ameuwawa kwa  kukatwa na  panga  sehemu  za kichwani ,mkononi na tumboni hadi utumbo wake  kutoka nje  na watu wawili wasiofahamika  kwa sura wla majina yao
Tukio hilo la mauwaji ya kusikitisha lilitokea hapo  june  29 mwaka huu majira ya saa mbili  usiku nyumbani kwa marehemu ambae alikuwa akiishi kijini hapo na familia yake
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa   nje ya nyumba yake  akiwa na  mke wake  aitwaye  Yulitha    Stephano (34) pamoja  na wasaidizi wake wakazi watatu wakijiandaa kula mlo wa usiku
 Wakati wakila chakula  ilitokea pikipiki  moja  ambayo ilikuwaimewabeba watu wawili  waliokuwa wamevaa makoti meusi walipofika walimsalimiaana  marehemu  na kisha walimweleza kuwa wao wametokea kijiji cha Mishamo lakini wanaishi Kijiji cha Kakese  na wamefika hapo kwa ajiri ya kutafuta eneo la kuchungia mifugo yao
Kamanda Kidavashari alisema marehemu  aliwajibu  kuwa maeneo yanapatikana yanapatikana hivyo walale  ilikesho yake asubuhi  ili aweze  kuwapeleka  kwa mwenyeji  ambae  anaweza  kuwapatia eneo la kuchungia mifugo yao
Baada  ya mazungumzo hayo  wageni hao  waliomba wapatiwe chakula na sehemu ya kulala  ambapo  wageni hao walitimiziwa ombi hilo na walipewa chakula na kisha waliandaliwa sehemu ya kulala
Kidavashari alieleza  wagani hao  baada ya kuonyeshwa sehemu ya kulala baadaye waliamka  na kwenda kwenye nyumba ambayo alikuwa amelele marehemu na mke wake  na  kisha walivunja mlango na kuingia ndani na kuanza kumashambulia marehemu kwa mapanga
Alifafanua ndipo mkewe alipoona mume wake anashambuliwa kwa mapanga alianza kupiga mayowe ya kuomba msaada kwa majirani hata hivyo wauwaji hao  walianza kumshambulia na yeye na kumjeruhi  kichwani
Alisema hata hivyo mke wa marehemu alifanikiwa  kukimbia  na kwenda kwenye nyumba  iliyokuwa kuwa jirani  waliokuwa wamelala  wasaidizi  watatu wa kazi wa marehemu  na kuwaeleza kilichotokea
Wasaidizi hao wa kazi waliamka na kuongozana na mke wa marehemu  ili kwenda kutoa msaada  na walipofika kwenye nyumba aliyokuwa amelala marehemu  walipoingia ndani  walikuta tayari ameishafariki  na wauwaji wakiwa wameisha tokomea  kusiko julikana na pikipiki yao
Kamanda Kidavashari alisema  katika tukio hilo  wauwaji  hawakutambulika  wala namba za pikipiki  hazikuweza kukaririwa  kutokana na wenyeji wao kutokuwa na mashaka juu ya watu hao  ambao muda wote  walikuwa  wamevaa kofia ngumu kichwani mwao (Helmet)
Alieleza  uchunguzi   wa awali  unaonyesha  chanzo cha  mauwaji hayo  kimetokana na kugombea mali kati ya marehemu  na familia ya mke wake mkubwa  aitwaye  Justina  Philipo kwani marehemu aliondoka  kwenye kijiji  cha Kakesa na kumwacho mke mkubwa na kuondoka na mke mdogo na kuhamisha mali zote zikiwemo Ng’ombe na mashine ya kusaga
Jeshi la polisi linamshikilia   Justina   Philipo na  mama yake mzazi    Kitola Simon kwa ajili ya mahojiano zaidi kuhusiana na  tukio hilo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa