Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Ka tavi
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima
amewataka vijana kujiunga
na mafunzo ya VETA kuanzia
waliomaliza elimu ya Msingi
ili wakape wawaze
kupata elimu ya kujiajiri
Mwamlima alitowa
wito huo hapo juz kwenye Kijiji cha Kasekese
Wilayani hapa wakati akifungua kambi ya vijana walijitolea kufyatua matofali kusomba mawe na mchanga kwa ajiri ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kumi ya shule ya Msingi
ya Kasekese na bweni la sekondari ya
Mpanda Ndogo
Alisema vijana wanawajibu wakutambua kuwa Taifa
la Tanzania linawategemea vijana kwa ajiri ya ujenzi wa nchi na sio wao
kulitegemea Taifa
Aliwafafanulia
kuwa mataifa yote Duniani yanajengwa
na yalijengwa na vijana hivyo
wanawajibu wa kuutumia vizuri ujana wao kwa sughuli za ujenzi wa Taifa
Alisema vijana wa Wilaya ya Mpanda wanayonafasi
kubwa ya kuanzisha shughuli
za kiuchumi kutokana na
furusa zilizopo Wilayani hapa
Alifafanua vijana
wengi katika Wilaya ya Mpanda hawana ardhi
hivyo vijiji vyote
vikae na kuwapatia ardhi vijana zoezi hilo lifanyike kwa ushirikiano baina ya
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na vijiji husika
Alieleza wako baadhi
ya vijana wamekuwa
wakimshangaa pale anapokuwa akiongelea vijana wapewe ardhi wanapaswa watambue kuwa rasilimali kubwa ya bara la Afrika ambayo ni yauhakika
ni ardhi
0 comments:
Post a Comment