Home » » AZIAGIZA HALMASHAURI KUZIELIMISHA JAMII KWA VITENDO ZIONDOKANE NA UMASKINI ILI KUONDOA UHALIFU

AZIAGIZA HALMASHAURI KUZIELIMISHA JAMII KWA VITENDO ZIONDOKANE NA UMASKINI ILI KUONDOA UHALIFU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi Paza Mwamlima ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ameziagiza Halmashauri  zote zilizopo katika Mkoa wa Katavi  zihakikishe  sekita zao  zinajikita  kuelimisha jamii kwa vitendo  ili ili kuondoa  umasikini kwa wakazi wa Mkoa wa Katavi
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi alitowa agizo hilo hapo jana wakati akifungua washa ya siku ya Polisi  iliyofanyika hapo juzi kwenye ukumbi wa Super City  uliopo mjini hapa
Mwamlimu alisema Mkoa wa Katavi umebahatika kuwa na furusa nyingi lakini  mpaka sasa hazijatumika ipasavyo  kutokana na  wananchi  kutoelewa umuhimu wa kuzitumia furusa hizo
Alisema wakati sasa umefika wa kila Halmashauri  kutafusili  furusa zilizopo katika Mkoa wa Katavi  ili ziweze  kuwanufaisha  wananchi kiuchumi na kuwaondolea umasikini hivyo wataalamu  wakikite  kwa wananchi  na kuwapatia elimu
Alifafanua   kuwa Wakurugenzi  wahakikishe wanashirikiana  na wafanya biashara  katika  kutafuta  masoko ya mazao  ya ndani  ya nchi na nje ya  nchi kwani  mazao mengi yamelundikana kwenye maghala  kutokana na kutokuwa  na kutokuwa na mbinu za wafanya biashara  ya kutafuta masoko ya kuuzia
Alisema  hari ya watu inapokuwa  mbaya kiuchumi  husababisha  kuwepo kwa uhalifu  hivyo ilikukabiliana na  uhalifu  ni vizuri  kuhakikisha hari ya uchumi kwa wananchi inakuwa nzuri
Alifafanua  ilinchi yetu iendelee  kuwa na amani  na usalama   ni vema  kukumbushana  na kutathimini  nini kinahitajika  katika kuimalisha ulinzi  na usalama  hapa nchini  kwetu
Alisema jeshi la pilisi  litafanikiwa kuondoa uhalifu  endapo wataacha kufanya kazi kwa mazoea  hivyo wanao wajibu   kubadilika  fikira  na kuleta tija 
Kwa upande wake mkuu wa Kitengo cha polisi jamii hapa nchini Kamishina wa Polisi Mussa Ally Mussa   alisema ni vema watu wakatambue kuwa kazi ya polisi jamii sio kazi ya polisi peke yao  hivyo wananchi wanao wajibu wakushirikiana na jeshi la polisi  kwenye jukumu zima la polisi jamii
Alisema dhamila ya polisi jamii sio  hasa  kupambana na  wahalifu  bali dhamila  kuu  ya polisi jamii ni  kuzuia uhalifu usitokea
Alieleza jeshi la polisi linakabiliwa na shangamoto mbalimbali  kama vile  uchache wa Askari pamoja na vitendea kazi mbalimbali  changamoto hii ambayo  inayakabili majeshi yote ya polisi  ya nchi zote duniani
Changamoto  nyingine aliitaja kuwa ni utovu wa  nidhamu kwa baadhi ya askari ambapo wapo wengi wamekuwa wakipokea rushwa kwa kisingizio cha mshahara  mdogo wakati sio kweli  kwani serikali imejitahidi kuboresha  mishahara ya askari kwa kuwapatia posho kila mwezi
Kamishina Mussa alieleza wapo baadhi ya Askari wamekuwa na tabia ya kuvuta sigara barabarani  huku wakiwa wamevaa  sare  za jeshi la Polisi  wakati ni kinyume cha utaratibu askari wanaofanya hivyo ni wahuni
Nae mmoja wa washiriki wa washa hiyo Thomas Ngozi alisema kuwa askari wa jeshi hilo wanaoajiliwa siku hizi wamekuwa hawana maadili kutokana na  askari wanao ajiliwa kuwa na umri mdogo hivyo  ni vema umri wa kuajiri ukaongezwa kutoka miaka 18 hadi miaka 20

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa