Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Charles
Mkimbili (60) wa Kijiji cha Kaulolo
Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi ameuwa
kwa kukatwa na shoka
kichwani na mtu asiyefahamika wakati
wakati akila chakula cha jioni na familia yake
Tukio hilo la mauwaji ya kinyama lilitokea
hapo juzi majira ya saa mbili usiku
kijini hapo nyumbani kwa marehemu Charles
Mkimbili
Kwa mujibu wa
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa
Katavi Kamishina Msaidizi Mwandamizi Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo lilitokea
nyumbani kwake na marehemu wakati akiwa anakula chakula cha
jioni akiwa na familia yake
Alisema wakati marehemu akiwa anakula chakula na familia yake ghafla
alitokea mtu mmoja mwanaume akiwa
amejifisha sura yake huku akiwa ameshika shoka mkononi
Kamanda
Kidavashari alieleza mtu
huyo baada ya kuwa kufika hapo
walipokuwa wakila chakula alianza
kumshambulia marehemu kwa kumkata na
shoka kichwani sehemu ya kisogo na usoni
huku familia yake ikiwa inapiga
matowe ya kuomba msaada kwa majirani
Alisema mtu huyo baada ya kuona mayowe yanazidi
aliamua kukimbia na kutokomea mahari kusiko julikana huku akiwa amebeba
shoka lale
Alifafanua majirani walifika kwenye eneo hilo na kumkuta marehemu akiwa amegalagala chini huku akiwa tayari ameisha
fariki Dunia na pembeni yake damu zikiwa zimetapakaa
Kamanda Kidavashari alisema
chanzo cha mauwaji hayo bado
hakijajulikana hivyo Jeshi la Polisi
linaendelea na upelelezi wa tukio hilo
na kuhakikisha linawatia mbaroni wahusika wa tukio
hili ili waweze kufikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria
Home »
» Auwawa kwa kushambuliwa na shoka wakati akila chakula na familia yake

0 comments:
Post a Comment