Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mkuu wa Wilaya ya
Mpanda Paza Mwamlima amewaagiza wazazi wa Wanafunzi wa shule ya
Sekondari
ya Mpanda Ndogo iliyoko Tarafa ya Kabungu Wilayani Mpanda
kuhakikisha
watoto wao walioacha shule kwa ajiri ya otoro na kwa kwasababu ya
kuowa na kuolewa wahakikishe watoto wao wanarejea shuleni hata kama
wamezaa watoto
Mkuu huyo wa
Wilaya alitowa agizo hilo hapo juzi
wakati wa mkutano
wa kamati ya maendeleo ya Kata
hiyo pamoja na wazazi wawanafunzi
wa wanaosoma kwenye shule hiyo ulifanyika shuleni hapo kwa lengo la kujali maendeleo ya shule hiyo
ambayo ilishika nafasi ya mwisho kwa ufaulu wa wanafunzi katika mtihani wa
kidato cha nne mwaka jana kwa shule za sekondari za Mkoa wa Katavi
Alisema shule
hiyo imekuwa na matokeo mabaya ya ufaulu
wa wanafunzi kutokana na utoro
uliokithiri kwa wanafunzi kuacha shule
kwa ajiri ya kuowa na kuolewa huku wazazi wao wakiona kuwa ni jambo la
kawaida
Mwamlima aliwaeleza Serikali ya Wilaya amepanga
kuendesha msako kwa kutumia jeshi la polisi mwezi Julai
kuwasaka na kuwakamata na kuwapeleka shuleni wanafunzi wote watoro na walioacha shule kwa kuowa na kuolewa hata
kama watakuwa wamezaa watoto watapelekwa
shule na watoto wao migongoni
Alisema ni vizuri
wazazi watowe ushirikiano katika zoezi hili ilikuweza kuipandisha shule hiyo na kuifanya ishike nafasi ya juu kwa ufaulu
wa wanafunzi kwani bila elimu wazazi wa wanafunzi hao wataendelea kuwa
masikini tuu aliwaeleza Mwamlima
Awali Mkuu wa Shule hiyo Rashid
Msyete alieleza kuwa shuhttps://draft.blogger.com/blogger.g?blogID=2686366488337348656#editor/target=post;postID=5788232012877525037le hiyo yenye kidato cha kwanza hadi cha nne
inawafunzi 165 kati yao wanaume ni 104 na wanawake 61 wakati uwezo wa shule hiyo ni kupokea
wanafunzi 600
Alisema kila
mwaka shule hiyo inapangiwa kupokea wanafunzi 120 kwa ajiri ya kujiunga na
kidato cha kwanza lakini wengi waao hawaripoti shuleni kutokana na mwamko mdogo wa wazazi katika swala zima la
elimu na kupelekea baadhi ya wazazi kuwaruhusu watoto wao kuolewa na kuowa
Kwa upande
wake mmoja wa wazazi wa wanafunzi
Cristopha Mkula alisema kuwa
wanafunzi wanao soma kwenye Sekondari hiyo walikuwa wanakatishwa
tamaa kutokana na shule hiyo kuwa na
waalimu wachache hari ambayo
ilisababisha wanafunzi kukosa baadhi ya
masomo na kuwafanya wawe watoro
Nae Verovika
Godfrey alieleza kuwa wanafunzi
wengi wa shule hiyo wamekuwa ni watoro kutokana na adhabu kali zinazotolewa na waalimu shuleni hapo
pindi mwanafunzi anapokuwa amefanya kosa
Alisema ipo
adhabu moja inayoitwa kunyonya mafuta
ndio imekuwa kikwanza kikubwa kwa wanafunzi kuwa watoro shuleni hapo kwani huwa inatolewa kwa
muda mrefu kwa mwanafunzi
Hata hivyo mkuu
wa wilaya Paza Mwamlima alimtaka mwanafunzi mmoja atowe ufafanuzi wa aina ya adhabu hiyo ya kunyonya mafuta ni
ya nanma gani ndipo mwanafunzi huyo alipo eleza kuwa edhabu hiyo huwa ni ya mwafunzi huwa anaambiwa aweke
kichwa chini ya ardhi huku miguu
ikiwa ijuu
Aidha diwani wa
Kata hiyo Hamad Mapengo alieleza kuwa
lile tatizo la upungufu wa waalimu
lililokuwepo awapo awali mwaka
huu limepungua sana baada ya Serikali kupeleka
waalimu mapema mwaka huu
0 comments:
Post a Comment