Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Askofu Gervas Nyaisonga
amesimikwa kuwa Askofu wa Kanisa Katoliki
Jimbo la Mpanda ambalolilikuwa
wazi kufutia kifo cha aliyekuwa
Askofu wa jimbo hilo Askofu Wiliamu Kikoti
aliyefariki Dunia tarehe
28 Agosti 2012
Ibada ya
kusimikwa Askofu Gervas Nyaisonga ilifanyika juzi kwenye
viwanja vya shule ya
chekechea inayomilikiwa na Kanisa
Katoliki Jimbo la Mpanda ambayo ilihudhuriwa
na maaskofu wapatao ishirini wa majimbo mbalimbali na viongozi wa Serikali
akiwemo Mke wa Waziri Mkuu
Tunu Pinda
Askofu Gervas Nyaisonga aliteuliwa na Baba mtakatifu Francisko
1 kuwa Askofu wa jimbo la Mpanda
hapo mwezi februai mwaka huu kabla ya
uteuzi huo i Askofu Gervas
Nyaisnga alikuwa ni Askofu
wa Jimbo la Dodoma ambalo ambalo
ameliongoza jimbo hilo kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2011
Katika salamu zaBaraza la
Maskofu
zilizotolewa na Rais wa Baraza
la Maaskofu Tanzania Askofu
Taransiunce Ngalalekumtwa alieleza kuwa Baraza la maaskofu
linaimani na Askofu Nyaisonga kuwa anao uwezo mkubwa wa kuliongoza
jimbo la
mpanda hivyo hawana mashaka na uteuzi
huo wa kuhamishiwa kwake kuwa Askofu wa jimbo hilo
Alisema Waumini wa kanisa hilo wa jimbo la Mpanda na wanachi
wanawajibu wa kumpa ushirikiano
Askofu Nyaisonga ili aewze kufanya kazi
zake vizuri
Kwa upande wake
mke wa waziri mkuu Mama Tunu Pinda alieleza kuwa anamfahamu vizuri Askofu Nyaisonga kuwa ni mpenda maendeleo
sana na mpenda watu hivyo wanampanda watarajie
yale ambayo yalikuwa yameanzishwa
na marehemu Askofu Kikoti yataendezwa nae hivyo kiatu alichokiacha Askofu Kikoti
kimepata mvaaji ambae ni Askofu
Nyaisonga Alisema Tunu Pinda
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengwe
alieleza kuwa Mkoa wa Katavi unarasilimali nyingi
lakini unakabiliwa na changamoto
mbalimbali ambazo zinahitaji ushirikiano
wa Serikali na kanisa ili kuweza kuzipunguza na kuzimaliza
Dr Rutengwe
alizieleza baadhi ya changamoto hizo ni
miundombinu mibovu ya barabara eimu
na Afya
ambapo mkoa wa Katavi mpaka sasa
hauna hospitali yake ya Mkoa wanategemea
Hospitali ya Wilaya ya Mpanda tuu
0 comments:
Post a Comment