Home » » ASKOFU NYAISONGA KUSIMIKWA KESHO KUWA ASKOFU WA JIMBO LA MPANDA‏

ASKOFU NYAISONGA KUSIMIKWA KESHO KUWA ASKOFU WA JIMBO LA MPANDA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na  Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Askofu  Gervas Nyaisonga (48 )anasimikwa kesho siku ya jumapili kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda  katika ibada inayotarajiw kufanyika kuanzia saa nne asubuhi  katika  viwanja vya shule ya chekechea inayomilikiwa na Kanisa Katoliki jimbo la Mpanda
kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa  na uongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda ibada ya kusimikwa  Askofu Nyaisonga  itahudhuriwa na Maaskofu wote wa Kanis hilo  na mapadri   watawa na walei wakutoka majimbo mbalimbali ya kanisa hilo
Askofu  Nyaisonga anahamia  jimbo Katoliki  la Mpanda kabla ya hapo alikuwa ni Askofu wa Jimbo la  Dodoma  jimbo la Mpanda lilikuwa halina Askofu toka mwaka juzi  kufuatia kufariki kwa aliyekuwa Askofu wa jimbo hilo Paskal Kikoti  kufariki Dunia hapo mwaka juzi
Jimbo Katoliki la Mpanda lilianzishwa mwaka 2001 na Askofu wake wa kwanza wa Jimbo hilo alikuwa ni  marehemu Paskali Kikoti hinyo Askofu Gervas Nyaisonga atakuwa ni Askofu wa PILI tangia jimbo katoliki la Mpanda lilipoanzishwa
Katika ibada hiyo ya kusimikwa kwa Askofu Nyaisonga Serikari itawakilishwa na Waziri wa Nchi ofisi ya waziri Mkuu uwekezaji na uwezeshaji Mery Nangu  ambae  atatowa salamu za Serikali kwenye ibada hiyo
Miongoni wa watakao hudhuria ibada hiyo   hapo kesho ni Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda na viongozi mbalimbali wa Serikali wa Mkoa wa Katavi na Viongozi wa mikoa ya jirani ya Rukwa Tabora na Kigoma

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa